In Summary

•Baada ya ushindi wa Senegal Jumapili usiku, rais wa nchi hio Macky Sall alitangaza Jumatatu kuwa siku ya likizo kusherekea taji la kwanza la  Kombe la mabingwa Afrika(AFCON) kufuatia ushindi wao dhidi y Misri.

 

Senegal wanyakua taji la kwanza la Afcon kwa kuibwaga Misri
Image: GETTY IMAGES

Baada ya ushindi wa Senegal dhidi ya Misri Jumapili usiku, rais wa nchi hio Macky Sall alitangaza Jumatatu kuwa siku ya likizo kusherekea ushindi wa taji lao la kwanza la  Kombe la mabingwa Afrika(AFCON) .

Kupitia runinga ya taifa, Sall alitangaza kuwa safari zote alizopanga kusafiri ameahirisha hadi sherehe hizo zifikie kikomo.

Rais huyo aliye mamlakani alipaswa kuzuru nchi ya Comoros Jumatatu lakini safari yake ilikatizwa baada ya ushindi mkubwa  dhidi ya Misri.

Sall alieleza kuwa alighairi nia, ili kubisha kuwa kuwakaribisha timu ya taifa watakapokuwa wakirejea nchi hio la Kombe la AFCON Jumatatu saa 12.

Senegal ilibwaga   Misri kupitia matuta ya penati ambapo waishinda 4-2.

Senegal ikiongozwa na nyota wa Liverpool sadio Mane walitangazwa  mabingwa wa AFCON  2021 kwenye fainali ya kuvutia macho  nchini Cameroon.

Ikumbukwe Senegal wameshindwa mara mbili katika fainali za awali mwaka wa 2002 na 2019 mtawalia.

View Comments