In Summary
  • Awali Serikali ya Ukraine ilisema kwamba imeomba Mahakama ya Kimataifa ya Haki kufungua mashtaka dhidi ya Urusi juu ya uvamizi huo
Image: REUTERS

Mapigano makali yaliendelea mwishoni mwa wiki, huku majeshi ya Urusi yakilenga miji kadhaa nchini Ukraine, lakini wakashindwa kuuteka mji muhimu wa Kharkiv kaskazini mashariki na ambo ndio mji mkuu wa pili.

Hatahivyo, mashambulizi kutoka kwa Urusi yanaendelea kutoka kila upande , na wanajeshi wa Urusi wanasemekana kupiga hatua kutokea kusini mwa Ukraine wakizingira miji ya Kherson na Berdyansk, maeneo mawili ya bahari nyeusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametangaza mipango ya kukutana na ujumbe wa Urusi katika mpaka wa Ukraine na Belarus baada ya mazungumzo na kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko. Hakuna ratiba iliyotolewa na hali inatia wasiwasi, kutokana na msaada wa Belarusi kwa Putin

Awali Serikali ya Ukraine ilisema kwamba imeomba Mahakama ya Kimataifa ya Haki kufungua mashtaka dhidi ya Urusi juu ya uvamizi huo.

Washirika wake wa Ulaya na Marekani wameishutumu serikali ya Urusi kwa kuongezeka kwa mvutano zaidi baada ya Rais Putin kukiweka tayari kikosi chake cha ulinzi wa nyuklia katika "tahadhari maalum".

Wakaazi katika mji mkuu Kyiv, bado wako chini ya amri ya kutotoka nje wakati mashambulizi zaidi katika mji mkuu huo yakiendelea, na ripoti za wanajeshi zaidi wa Urusi wakielekea katika mji huo.

Warusi wako tayari kwa mgogoro wa kifedha kabla ya masoko kufunguliwa Jumatatu baada ya vikwazo vikali kutangazwa mwishoni mwa wiki ambavyo vitazizuia benki za Urusi kutumia mfumo wa kifedha wa kimataifa.

 

 

 

 

 

 

 

View Comments