In Summary

• Mkimbizi huyo alisema walitoroka Afghanistan kuenda Ukraine kwa sababu ya vita vya Talibani.

• Chini ya miezi sita baadaye tena Urusi inazua vita Ukraine na kuwabidi watoroke kwenda Uingereza.

• Uingereza inataka kuwahamisha wakimbizi wote kuja Afrika ambapo wameteta vikali kuwa Afrika ni mateso tupu.

Mkimbizi na mhanga wa vita nchini Afghanistan amezua gumzo mitandaoni baada ya shirika la habari la Sky nchini Uingereza kupakia video ya mahojiano yake akikejeli bara lote la Afrika kwamba ikiwa wakimbizi hao wataletwqa humu basi maisha yao yatavurugika zaidi ya yalivyovurugwa na vita nchini kwao kwani kulingana na yeye maisha katika bara la Afrika hayana matumaini kabisa.

Raila huyo wa Afghanistan pamoja na wengine walikimbia nyumbani kwao mwaka jana wakati kundi la kigaidi la Taliban lilipotwaa uongozi wa taifa hilo la Mashariki ya kati na kukimbilia Poland, Germany, Ufaransa na ambapo walijipata wameingia nchini Ukraine.

Chini ya miezi sita tu baada ya kukimbia vita nyumbani kwao Afghanistan, nchini Ukraine walikokimbilia pia vita vilizuka kule ambapo majeshi ya Urusi yalishambulia nchi hiyo kwa kile walidai kwamba Ukraine inataka kujiunga na muungano wa NATO, kinyume na matakwa na Urusi.

Kutoka Ukraine tena wakimbizi hao walihamia nchini Uingereza kwa njia zisizo halali na sasa Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kwamba wakimbizi wote wa aina hiyo watahamishiwa nchini Rwanda, Afrika.

Tamko hilo la Johnson lilionekana kumghadhabisha raia huyo wa Afghanistan ambaye aliteta vikali kwamba iwapo wataondolewa Uingereza basi haifai kuletwa Afrika kwani huku hakuna imqani kabisa.

“Maisha yetu yalikuwa hatarini nyumbani Afghanistan, sasa wakitupeleka Afrika ni nini tunaenda kufanya kule? Hakuna mustakabali wa maisha kule Afrika, unajua tumetoka Afghanistan na hatuwezi ishi kule kwa sababu Taliban tayari wametawala. Tumetorokea huku na wadogo zetu kwa sababu tunataka kufanya vitu katika maisha yetu ya kesho, tuna mengi yanayotusubiri mbeleni katika maisha, sasa kama watatuhamishia Afrika tutaenda kufanya nini kule? Watu Afrika wanateseka, wanaumwa na njaa hadi kufa, hilo la kutupeleka kule halileti maana kabisa, ni kama kutuhukumu mara mbili. Haifai kuwa hukumu mara mbili duniani,” raia huyo wa Afghanistan aliteta vikali.

View Comments