In Summary

•Hatua hii inakuja siku moja baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanza majadiliano na Kampuni ya Meta inayomiliki mitandao ya Faceboo

Image: BBC

Serikali ya Tanzania inaendelea na mchakato wa kuandaa utaratibu wa kutoza kodi watumiaji wote wa mitandao ya kidijitali ambao wanafanya biashara bila ya kulipa tozo hiyo halali ya umma.

Hatua hii inakuja siku moja baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanza majadiliano na Kampuni ya Meta inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp kwa lengo la kuanza kukusanya kodi katika zitokanazo huduma zake nchini.

Akizungumza na BBC jijini Dar es Salaam,Richard Kayombo ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo, alisema kuwa zoezi hilo litakapokamilika, kodi hiyo haitatozwa kwa wale wanaotumia mitandao kwa matumizi yasiyoingiza kipato.

“ Watanzania wawe watulivu, hatutawatoza watu ambao hawafanyi biashara mitandaoni. Sisi tutakaowatoza hapo mbeleni ni wale wanaofanya biashara kwenye mitandaona ndio maana timu ya wataalamu wa Kampuni ya Metawaimefanya mazungumzo ya awali na TRA kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma zao nchini,” Kayombo ameeleza na kuongeza kuwa;

“Baada ya mazungumzo hayo ambayo Meta wametupa uzoefu wao katika kuchangia kodi kwenye nchi kama Kenya, Nigeria na Afrika Kusini, sasa Serikali inaendelea kuangalia upande wa sheria zetu ili tuone namna gani tunaweza kuanza kukusanya kodi kwa wale wanaofanya biashara mitandaoni.’

Mpaka Desemba 2021,Tanzania ina watumiaji zaidi ya milioni 29 wanaotumia intaneti.

View Comments