In Summary

•Mashahidi walisema waliona Bw Musengimana "akimpiga kwa nguvu nguruwe huyo kwa kipande kikubwa cha mbao"

Image: GETTY IMAGES

Mahakama moja mashariki mwa Rwanda imemhukumu Imam Mwislamu kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua nguruwe msikitini.

Sadate Musengimana alikubali kumuua nguruwe huyo 'kwa bahati mbaya' mwezi Februari alipofika karibu na msikiti na "kuvuruga mafundisho yake ya quran", waraka wa mahakama unasema.

Mashahidi watatu waliambia mahakama kwamba waliona Bw Musengimana "akimpiga kwa nguvu nguruwe huyo kwa kipande kikubwa cha mbao" na kumuua papo hapo, waraka ulioonekana na BBC unasema.

Yusuf Nsengiyumva, wakili wa Bw Musengimana, analaani "hukumu kali" kwa mteja wake akisema alimuua mnyama huyo kwa bahati mbaya.

"Watoto walipopiga kelele kwa kuona nguruwe msikitini, alitoka nje ili kumfukuza kwa fimbo, alimpiga na akafa, lakini hakuwa na nia ya kumuua", Bw Nsengiyumva aliambia BBC.

Upande wa mashtaka ulikuwa umeomba kifungo cha miaka saba jela dhidi ya Bw Musengimana, huku utetezi wake haukuona sababu yoyote ya kifungo cha miaka mitano jelaikiwa ni mara moja zaidi kupatikana na hatia ya kuua mnyama wa kufugwa kwa nia mbaya katika sheria za Rwanda.

Raia wa Rwanda kwenye mitandao ya kijamii na vikundi mbalimali wameonyesha mshtuko kujua hatima ya Bw Musengimana ilipotoka kwenye vyombo vya habari wiki jana.

Wakili wake aliambia BBC kwamba wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama, huku Bw Musengimana akiwa gerezani tangu Februari alipomuua nguruwe huyo.

View Comments