In Summary

• "Kufanya ukatili kama huu wa kusitisha maisha ya mtoto ni jambo la kutia uchungu" - Mkuu wa polisi Mwalukasa.

Tukio lisilo la kawaida lilitokea Jumanne katika mji wa Mbeya Tanzania baada ya mtoto mchanga kupatikana ametupwa kwenye jalala la taka na kuliwa na mbwa kuanzia kiunoni Kwenda chini miguuni.

Katika tukio hilo la kusikitisha, watu waliokuwa wanaelekea eneo hilo la kutupa taka walishtushwa baada ya kuona kijusi hicho kimetupwa hapo na tayari kilikuwa kishaliwa na mbwa wanaoranda usiku wakisasambura mapipa ya taka kwa ajili ya chakula ambacho walikipata na kukila mwili nusu.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba kwa haraka haraka inaonesha mtoto huyo huenda alitupwa usiku wa kuamkia jana huku akiwa amewekwa katika mfuko wa plastiki na kichanga hicho kimeliwa na Mbwa kuanzia kiunoni kushuka chini.

Kwa upande wake, Nimbwelu Mwalukasa mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya Mjini amethibitisha kwa tukio hilo na kuomba ili kuweza kumbaini mtu aliyehusika na tukio hilo.

“Matukio kama haya huwa yanasikitisha sana, ni kitendo amabcho sisi kama wanawake hata wanaume pia inasikitisha na inatia uchungu sana. Kufanya ukatili kama huu wa kusitisha maisha ya mtoto, mtoto ambaye hatujui kesho angekuja kuwa mtu wa msaada katika eneo hili si jambo la kufurahisha, huenda tunasikitika hapa lakini kuna mtu anamjua aliyeavya kijusi hiki na kukitupa hapa, tunaomba ushirikiano wenu ili tumpate,” Mwalukasa alizungumza kwa uchungu wa mama.

Kitendo hicho cha kusikitisha kiliwachukiza wengi ambao waliapa kushirikiana na polisi ili kumtia nguvuni mwanamke mshukiwa ambaye aliavya mimba hiyo na kuitupa jalalani. Wengine walionesha kusikitishwa kwao kwa vitendo kama hivyo kwani vimekithiri sana hali ya kuwa kunao wengi wanaotafuta watoto pasi na mafanikio.

“Yesu wengine tunavyowatamani hivi, Mungu awasamehe kama humtaki mtupe sehemu nzuri anapoweza saidiwa na watu bila kudhulika jamani,” mmoja alisema.

View Comments