In Summary

• Ilisemekana kwamba askofu huyo alikuwa amekula kiapo cha kuhudumu kama askofu siku sita tu kabla ya kifo chake.

Askofu George Chiteto wakati wa kuapishwa kwake kama askofu
Image: YouTube screengrab

Moja ya taarifa za tanzia amabazo zimezungumziwa sana na Wakristo waumini katika ukanda wa Afrika Mashariki ni kifo cha askofu mmoja wa kanisa la Kianglikana nchini Tanzania.

Askofu huyo George Chiteto kutoka dayosisi ya Mpwapwa kifo chake kimezungumziwa sana haswa ikizingatiwa kwamba alikuwa amevishwa cheo cha uaskofu siku sita tu kabla ya kifo chake.

Kingine ambacho kilizua majonzi zaidi kweney mitandao ya kijamii ni uhalisia kwamba alifariki muda mchache tu baada ya kuongoza ibada ya mazishi ya mke wa askofu mwenzake.

Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba Askofu Chiteto alipatwa na mshtuko wa moyo na kukata roho alipokimbizwa katika hospitali moja nchini Tanzania.

Nchini Tanzania, hii si taarifa ya kwanza kwa mtumishi wa Mungu kufariki akiwa anaongoza ibada ya msiba kwani miezi miwili iliyopita kasisi mmoja wa kanisa Katoliki pia alifariki akiwa anaongoza ibada ya mazishi.

Kasisi huyo kwa jina Laurence Milanzi wa kanisa Katoliki kijiji cha Liputu, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, alifariki Dunia maeneo ya Makaburini alipokuwa akishiriki mazishi ya mwanakijiji mwenzao aitwae Daudi Veno.

Waliuoshuhudia tukio hilo la kusikitisha na kuchapisha taarifa hizo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii walisema kasisi Milanzi alianguka ghafla waakti alipokuwa akiwazungumzia watu umuhimu wa kuhudhuria misiba ya wenzao pindi wanapotangulia mbele za haki.

 

View Comments