Spika wa bunge Anita Among amesema kuwa bunge halitaruhusu kukuza utalii kwa kuwaweka hatarini watot
Image: BBC

Bunge la Uganda limeagiza kuwa tamasha linalofahamika kama Nyege Nyege, lililotarajiwa kudumu kwa siku tano ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika katika kipindi cha siku tisa katika wilaya ya mashariki mwa Uganda ya Jinja, lisitishwe.

Katika kikao cha bunge kilichokaa mchana huu, baadhi ya wabunge walisema kuwa tamasha hilo linaeneza uasherati.

Waziri wa utalii nchini humo, Martin Magara hatahivyo alitetea tamasha hilo alilolielezea kama kitovu cha utalii.

Alisema kuwa zaidi ya watalii 8000 tayari wamenunua tiketi kwa ajili ya tukio hilo.

Spika wa bunge Anita Among amesema kuwa bunge halitaruhusu kukuza utalii kwa kuwaweka hatarini watoto.

Waziri wa Maadili na Uadilifu alikuwa ametoa idhini ya tamasha hilo kufanyika kwa misingi kwamba watoto hawataruhusiwa kuhushuria na kwamba hakuna yeyote atakayekwenda kwenye tukio hilo akiwa uchi.

Hii si mara ya 7 kwa tukio la Nyege Nyege kufanyika nchini Uganda.

Tamasha hili ni la maonyesho zaidi ya muziki wa kielekroniki kutoka maeneo mbali mbali ya bara la Afrika pamoja na wasanii kutoka diaspora.

Wanamuziki kadhaa walitarajiwa kucheza mziki wao katika tamasha hilo.

Tamasha la Nyege Nyege sio mara ya kwanza kukumbwa na utata.

Mwaka 2018, serikali ilifuta tamasha hilo kwa misingi kuwa lilikuwa linakuza uasherati lakini ikaliruhusu baadaye baada ya malalamiko ya umma.

View Comments