In Summary

•Katika eneo hilo dogo , mwili wa babake malkia Elizabeth wa pili , Mfalme George  wa sita Pamoja na mamake Elizabeth Bowe – aliyejulikana kama Mama malkia – na dadake Mareret wamezikwa. 

•Mabaki ya mwanamfalme Phillip wa Edinburgh, Mumewe Elizabeth II kwa zaidi ya miaka 73 na ambaye alifariki mwezi Aprili 2021.

Kanisa hili la Mtakatifu George ndio lenye makaburi ya wafalme
Image: GETTY IMAGES

Baada ya kusafiri kwa zaidi ya kilomita 500 na kupokea heshima ya takriban viongozi 100 wa mataifa mbalimbali  kutoka kote duniani na mamia ya maelfu ya raia waliosubiri katika foleni kwa zaidi ya saa 1 , Mwili wa malkia Elizabeth utawasili jana Jumatatu kwa maziko.

Maziko yake yalifanyika katika kaburi la Kasri la Mfalme George huko Windsor.

Katika eneo hilo dogo , mwili wa babake malkia Elizabeth wa pili , Mfalme George  wa sita Pamoja na mamake Elizabeth Bowe – aliyejulikana kama Mama malkia – na dadake Mareret wamezikwa. Kaburi hilo liko karibu na kanisa la St George, Eneo ambalo idadi kuwa ya wafalme huzikwa katika ufalme huo wa Uingereza.

Mabaki ya mwanamfalme Phillip wa Edinburgh, Mumewe Elizabeth II kwa zaidi ya miaka 73 na ambaye alifariki mwezi Aprili 2021, pia yatahamishwa katika eneo hili dogo.

Mabaki ya Felipe  yalikuwa yamewekwa katika katika eneo la ifalme la kanisa la San Jorge Chaple  na sasa yatahamishwa ili kuzikwa na mkewe.

Kanisa la kumbukumbu la mfalme George VI, ambalo linafanya kazi kama kiambatisho, lilijengwa mnamo 1969 kwa agizo la Elizabeth II, na wazo kwamba sio mabaki ya wazazi wake tu, bali pia yake na yale ya mwanamfalme Philip yatapumzishwa hapo watakapo kufa .

Mahali hapo kuna mchoro wa dhahabu na picha ya babake Elizabeth II na, kwenye sakafu, kuna bamba jeusi lenye herufi za dhahabu ambapo majina ya mfalme George VI na Mamake Malkia na miaka inayolingana ya kuzaliwa na kifo imechorwa.

Lakini malkia Elizabeth wa pili hatozungukwa na familia yake pekee, lakini pia historia yote iliopo katika eneo hilo karibu nae neo la maziko yake kanisa la kifalme la Sant George.

Kaburi la Wafalme

St George's Chapel, iliyopo kando ya Kasri la Windsor - labda  ndio makao ya kifalme ambapo Elizabeth II alitumia muda wake mwingi - sio tu mahali pa sala.

Inatambuliwa kama mfano mashuhuri wa usanifu wa Kiingereza wa Gothic, katika miundo yake yote ni makaburi ya Wafalme tisa wa Uingereza, pamoja na wawakilishi wengi wa kifalme.

Kiasi kwamba imeipita Abbey maarufu ya Westminster kama sehemu yenye idadi kubwa ya makaburi ya washiriki wa ufalme wa Uingereza.

Ingawa Kasri la Windsor lilianzia karibu karne ya 11, kanisa lenyewe liliamriwa na Edward IV mnamo 1475, na miaka minane baadaye akawa mfalme wa kwanza kuzikwa hapo.

Kasri la Windsor, mojawapo ya maeneo yanayopendwa zaidi na Elizabeth II, itakuwa mahali pa mwisho pa mfalme huyo aliyetawala kwa miaka 70.
Image: BBC

Kazi ya ujenzi ilikamilishwa mnamo 1528, wakati mpango wa Henry VIII wa jumba la kanisa ulikamilishwa.

Kwa kweli, Henry VIII, mmoja wa wafalme wanaojulikana zaidi katika historia ya Uingereza, pia amezikwa hapa.

Moja ya sekta kuu ya kanisa la San Jorge ni kile kinachoitwa vault ya kifalme, ambayo iko chini ya nave ya kati.

Kuna makaburi ya wafalme watatu: George III, George IV na William IV, pamoja na washiriki wengine 21 wa kifalme, akiwemo Princess Alice, ambaye alikuwa mama wa Prince Philip wa Edinburgh.

Lakini katika pembe zingine za kanisa hilo kuna makaburi ya wafalme zaidi, kama vile Charles I, ambaye alikatwa kichwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Kiingereza (1642-1651), Henry VI, ambaye aliongoza moja ya kazi maarufu za mwandishi wa kucheza wa Kiingereza William Shakespeare. , na George V.

Agizo la Garter na harusi nyingi

Walakini, kwa wataalam wengi, kanisa, zaidi ya kuhifadhi mabaki ya washiriki wa kifalme, lina umuhimu wa kihistoria kwa sababu ndio mahali ambapo washiriki wapya wa Agizo la Garter watazinduliwa.

Agizo hilo, ambalo malkia Elizabeth wa pili anatoka na pia mfalem wa sasa Kinga Charles III, ni muhimu zaidi katika Ufalme huo wa Uingereza: Linatokana na kundi dogo la watuwaliochaguliwa na afisa wa ufalme huo.

Na mikutano yao pamoja na sherehe za matambiko ambayo yalioanza miaka ya katikati – hufanyika katika kanisa hilo la Saint George , ambaye mtakatifu wake ndio kiongozi wa kanisa la Uingereza.

Na kuna zaidi: Mbali na kuwa kitovu cha heshima muhimu kwa taji hilo, kanisa hilo limekuwa moja wapo ya sehemu zinazopendwa zaidi za harusi za kifalme.

Labda maarufu zaidi ambayo imefanyika hivi karibuni ilikuwa ile ya wanawafalme wa Sussex, Harry na Meghan Markle, mnamo 2018.

Vilevile, Edward, mtoto wa mwisho wa Malkia Elizabeth II, pia alimuoa Sophie Rhys-Jones na, karne moja mapema, Edward VII alimuoa Alexandra wa Denmark, ambaye angekuwa malkia wake.

Eneo hilo ambalo limejaa historia litakuwa eneo la mwisho la Isabel II, baada ya kuaga miaka 70 ya utawala wake.

View Comments