In Summary

•Mkanyagano huo ulitokea baada ya polisi kuwarushia vitoa machozi wafuasi waliokuwa wamezua ghasia.

•Video zinaonyesha mashabiki wakikimbia uwanjani baada ya kipenga cha mwisho.

Magari ya polisi yaliyoharibika yakiwa uwanjani ndani ya uwanja wa Kanjuruhan i yaliyoharibika yakiwa uwanjani ndani ya uwanja wa Kanjuruhan
Image: BBC

Takriban watu 129 wamefariki katika mkanyagano kwenye mechi ya kandanda ya Indonesia, maafisa wanasema, katika mojawapo ya maafa mabaya zaidi ya viwanja duniani.

Mkanyagano huo ulitokea baada ya polisi kuwarushia vitoa machozi wafuasi waliokuwa wamezua ghasia.

Takriban 180 walijeruhiwa katika mchuano huo baada ya Arema FC kushindwa na wapinzani wao Persebaya Surabaya huko Java Mashariki.

Waziri mkuu wa usalama wa nchi hiyo alisema kuwa idadi ya watazamaji ilizidi uwezo wa uwanja huo kwa takriban watu 4,000.

Rais Joko Widodo ameamuru kwamba mechi zote za ligi kuu ya Indonesia lazima zisimamishwe hadi uchunguzi utakapokamilika.

Video zinaonyesha mashabiki wakikimbia uwanjani baada ya kipenga cha mwisho.

Polisi kisha walirusha vitoa machozi, na kusababisha msongamano wa watu na visa vya kukosa hewa, alisema Nico Afinta, mkuu wa polisi katika Java Mashariki.

"Ilikuwa machafuko. Walianza kuwashambulia maafisa, wakaharibu magari," alisema na kuongeza kuwa maafisa wawili wa polisi walikuwa miongoni mwa waliofariki.

"Tungependa kueleza kuwa... si wote walikuwa wakorofi. Ni takriban 3,000 tu walioingia uwanjani," alisema.

Mashabiki waliokimbia "walikwenda kwa hatua moja wakati wa kuondoka. Kisha wakakusanyika pamoja, katika mchakato wa mkusanyiko kulikuwa na upungufu wa kupumua, ukosefu wa oksijeni", aliongeza.

Video kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mashabiki wakipanda juu ya uzio ili kutoroka. Video tofauti zinaonekana kuonyesha miili isiyo na uhai sakafuni.

Fifa, shirikisho la soka duniani, linasema kuwa hakuna "gesi ya kudhibiti umati" inapaswa kubebwa au kutumiwa na wasimamizi au polisi kwenye mechi.

Chama cha soka cha Indonesia (PSSI) kimesema kimeanzisha uchunguzi, na kuongeza kuwa tukio hilo "limetia doa uso wa soka la Indonesia".

View Comments