In Summary

•Javier Roca alisema vurugu kwenye mechi hiyo huko Java, ambapo watu 125 walipoteza maisha, "kumemvuruga akili"

Image: BBC

Mashabiki wa soka "walifia mikononi" mwa wachezaji wakati wa hekaheka za ajali kwenye uwanja wa Kanjuruhan nchini Indonesia, kocha wa timu ya nyumbani amesema, huku idadi ya watoto waliofariki katika mkasa huo ikiongezeka hadi 32.

Javier Roca alisema vurugu kwenye mechi hiyo huko Java, ambapo watu 125 walipoteza maisha, "kumemvuruga akili".

Mamlaka inasema mwathiriwa mdogo zaidi wa maafa hayo ya Jumamosi alikuwa miaka 3.

Naibu waziri wa masuala ya watoto na wanawake wa Indonesia alisema watoto waliopoteza maisha katika kukanyagana huko walikuwa na umri wa kati ya miaka 3 na 17.

Maafisa 18 wanachunguzwa baada ya polisi kuwarushia mabomu ya machozi mashabiki waliovamia uwanja mechi ilipomalizika.

Watu wengine 320 walijeruhiwa huku wafuasi hao kwa kukanyagana wakati wakikimbia huku na huko wengine wakizidiwa na hewa nzito ya moshi wa mabomu hayo ya machozi.

Shahidi mmoja aliiambia BBC kwamba polisi walikuwa wakirushwa mabomu mengi ya machozi "mara kwa mara na kwa haraka" kwa lengo la kuzuia mashabiki kuvamia uwanja. Hali ilikuwa "tete".

Wafuasi wa timu ya nyumbani ya Arema FC walivamia uwanja mara baada ya mechi kumalizika kuonyesha kutofurahishwa kwao kwa timu yao kuchapwa 3-2 na wapinzani wao Persebaya Surabaya

View Comments