In Summary

• Vijana ambao hawataki kurudi kwenye eneo la vita wanakubali kufungwa, kwenda kwenye kliniki za magonjwa ya akili au kuvuka mpaka na kukimbilia nchi nyingine.

Wanajeshi wa Urusi
Image: EPA

Watumishi wa jeshi wa zamani ambao waliachiliwa kutoka kwa jeshi la Urusi katika miezi ya kwanza ya vita na kutumikia chini ya mkataba sasa wanaitwa kwenda katika mstari wa mbele vitani kulingana na sheria za kuwasajili wanajeshi wa ziada.

Vijana ambao hawataki kurudi kwenye eneo la vita wanakubali kufungwa, kwenda kwenye kliniki za magonjwa ya akili au kuvuka mpaka na kukimbilia nchi nyingine. Waliiambia BBC kwa nini walifanya hivyo.

Mimi ni mlenga shabaha kwa taaluma. Yaani mimi binafsi sikuua mtu yeyote nikiwa na bunduki mkononi.

Kazi yangu ilikuwa kama hii: Kuwatafuta maadui kwa kutumia darubini inayoratibu , kabla afisa mwenzangu kulipata lengo, na baadaye mimi huelekeza macho na kushambulia, si vigumu kufanya. Katika sanaa ya ufundi wanakuambia "lengo liko tayari" - na ndivyo hivyo.

Je mafunzo hayo hufanywa wapi?

Huenda wanafunza hilo jeshini, lakini hakuna kitu kama hicho nilifanya. Katika kipindi cha kandarasi, tulitoka nje ya kitengo cha jeshi mara mbili – kuendesha magari na kulenga shabaha. Hatushambulii mahala popote.

Inaonekana kwamba ulifyatua risasi ulipoingia katika eneo la Ukraine kwa mara ya kwanza maishani mwako.

- Ndiyo. Kwa mara ya kwanza, tulienda Bucha.

- Kwa hivyo hii ni mara ya kwanza uko kwenye vita - mara ya kwanza katika maisha yako ulifyatua risasi huko?

- Ndiyo.

Sergey mwenye umri wa miaka ishirini kutoka Krasnadar hapo awali alizungumza na BBC. Mnamo Julai, alitoroka kutoka katika kambi yao hadi Popasna, alikaa nyumbani kwa miezi kadhaa na hakumwambia mtu yeyote jinsi alivyopigana kwa miezi mitano.

Mnamo Septemba 23, mwendesha mashtaka wa kijeshi alimpigia simu na kusema: "Ama utaenda huko tena Jumatatu, au utakamatwa." "Siko tayari kurudi," Sergey anasema. Wakati wa miezi mitano ya vita, alikuwa "ameona karibu kila kitu na hakuweza kuendelea zaidi."

Kifaru kilichoshambuliwa na kuharibika
Image: AFP AND GETTY IMAGES

'Hakuna malengo hakuna mipango'

Sergei mwenye umri wa miaka kumi na tisa alisajiliwa katika jeshi katika majira ya baridi ya 2021 na akajitolea kusaini mkataba mnamo Agosti: katika miaka ya hivi karibuni, Wizara ya Ulinzi imekuwa ikiwahamisha vijana wengi iwezekanavyo kwa aina hii ya huduma. Nambari zilikuwa muhimu kwa ripoti ya idadi ya wanajeshi waliohitimu katika jeshi.

Mwisho wa mwezi Januari, alitumwa Belarusi kwa mafunzo pamoja na wenzake, mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 18. "Tuligundua kuwa tulikuwa tukienda Ukraine mnamo Februari 23," anasema Sergey. Wanajeshi  waliambiwa kwamba "ikiwa hakuna kitu kitaamuliwa huko ifikapo jioni," basi kila mtu angeondoka. Na wakawapa chakula kikavu kwa siku tatu.

- Je, haikuwezekana kutoroka?

- Hakuna mahali pa kukimbia.

 

Walikwenda Chernobyl bila kufyatua risasi ndani ya vifaru "bora, vilivyotengenezwa kwa ufundi wa hali ya juu , Shambulio la kwanza lilitokea Gostomel - kikosi cha watu wapatao 600 kilipigwa na makombora ya silaha za UKraine: "Dakika hiyo maiti tano na ghafla watu kadhaa walijeruhiwa, hata wale waliokuwa wameketi ndani ya vifaru  - walipigwa. BMP-2 ni nyembamba na ni rahisi kuingiwa na."

Siku hiyo, Sergey aliona mtu aliyekufa kwa mara ya kwanza: Mwanajeshi mwenzake wa miaka 19, ambaye alihudumu naye huko Krasnadar, alikufa.

“Msisimko ulianza, hofu ikatanda, na ghafla tukaelekea Eneo fulani msituni, tukasimama na kuchanganyikiwa kabisa, hatukujua tufanye nini kama mabubu, makamanda hawakujua la kufanya pia. Kamanda wa kikosi akapiga kelele. kwa makamanda: [mbona] mumesimama tu!" - kisha wakatuambia "tuchukue msimamo".

Kikosi cha Sergeygil "kilichimba mahandaki kadhaa" na kukaa usiku kucha msituni. Sio tu kwamba walishambuliwa siku hiyo - kulingana na Sergey, askari wa Ukraine "walikishinda kabisa kikosi hicho " na wakati wa usiku waathirika walijificha "mahali fulani, kwa namna fulani" msituni. "Wetu walianza kuwafyatulia risasi. Walipiga mayowe." Kulingana na Sergey , ni mtu mmoja tu aliyejeruhiwa wakati huo.

"Asubuhi, tulikwenda kilomita chache hadi msitu mwingine. Waukraine walilipua ghala ambalo kambi ya kwanza ya jeshi ilikuwa wakati huo," anaongeza. (BBC ina video ya mashambulizi).

Makamanda hawakuwa na malengo, hakuna mipango, Sergey alisema. Hatukuwa na hata chakula, tulitumia chakula kikavu kilichotolewa kwa siku tatu kwa kiasi cha wiki.

"Hakuna aliyeeleza kwa nini hakukuwa na chakula. Makamanda wetu hawakula pia. Sijui kamanda wa jeshi, lakini wana kikosi cha upelelezi kinachosafisha hifadhi yote, kwa hiyo walikula kushiba, nadhani."

'Tulifyatua risasi'

Katika siku za kwanza za Machi, kikosi cha Sergey kiliingia Bucha: "Tulisaidia wanajeshi wa ardhini na  silaha. Tulisimama katikati ya jiji na kuwacha mizinga." Na nusu saa baadaye, ganda lilianguka mahali pao: "Wakati huo, makamanda wawili wa jeshi, kamanda wa kikosi na kikundi cha wanajeshi wa kawaida waliuawa," Sergey anasema.

Hapo mwanajeshi mwengine aliyehudumu na Sergey aliuawa karibu na Krasnodar

 

Akifa kamanda, mpya anateuliwa kutoka miongoni mwa waliosalia. Wakati huo huo, kuna watu wachache wenye uzoefu katika mstari wa mbele: Mara nyingi kila mtu ana umri wa miaka 19-20, Sergey anasema. "Kulikuwa na makamanda wa silaha adimu ambao walifanya kazi nzuri. Kamanda wetu wa bunduki alitumikia miaka 12, lakini hakuwahi jeshini, alikaa tu kwenye kitengo.

Huko Bucha, askari walianza kupora nyumba tupu na maduka: "Tangu mwanzoni, hakukuwa na chochote cha kula, tulichukua chakula cha makopo na mkate." Waliishi katika vyumba vya chini vya majengo ya ghorofa nyingi - wakaazi wa eneo hilo kwa upande mmoja, jeshi la Urusi kwa upande mwingine.

"Iwapo wakazi wa eneo hilo wangekuja kwenye Eneo letu , wangewakamata, kuwahoji na kuwaua mara moja. Wangeweka alama ya eneo letu kwenye simu na kutuma kwa Jeshi la Ukraine. Ilitokea kwmaba mtu mmoja anayepeleka baiskeli angepita karibu yetu na kuturekodi kupitia simu yake na kisha kutuma picha hizo kwa jeshi la UKraine. Baada ya dakika moja moto wa manjano ungeelekezwa kwetu Ndio. Lakini wanajeshi wetu walimkamata na kumuua mara moja , anasema Sergey.

View Comments