Daraja la Klitschko bridge mjini wakati mlipuko ulipotokea
Image: REUTERS

Katika kipindi cha saa chache kumeshuhudiwa mawimbi na mawimbi ya milipuko, sio yu hapa mjini Kiev, lakini pia katika maeneo mbali mbali ya nchi hii, kutoka Lviv magharibi mwa Kharkiv mashariki mwa ina Odesa katika kusini.

Kwa wengine wetu ambao tulikuwa hapa wakati Urusi ilipoanza uvamizi mwezi wa Februari, kuna kuzowea hali ya mashambulizi. Tumeambiwa kunapaswa kutumia muda mwingi kadri tuwezavyo kuwa katika vyumba vya chini vya majengo, kwani mashambulio zaidi, ya kutumia makombora na ndege zisizokuwa na rubani yanatarajiwa.

Lakini hii ni tofauti. Milipuko hapa Kyiv iko karibu zaidi na katikati mwa mji. Sio mbali na maeneo ya makazi ya watu, lakini, sauti kubwa za milipuko karibu na mitaa na maeneo ni sawa na ile ambayo tumeizowea kwa kipindi cha miezi minane iliyopita.

Ni vigumu kuelezea ni wapi kunalengwa, lakini taarifa kutoka katika wizara ya utamaduni ya Ukraine inasema majumba ya makumbusho na muziki yamepigwa kwa makombora.

Video moja inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha shimo kubwa katika uwanja wa michezo wa watoto.

Nyingine ilionyesha mlipuko wa kombora ukipiga daraja la vioo la Mayor Vitali Klitschko 'eneo maarufu la utalii na kituo kinachotumiwa na watu kuutazama mto Dnipro River kwa juu.

Olena na Valerii Badakh anaishi katika gorofa iliyopo kando na uwanja wa michezo katika Shevchenko Park.

"Ilikuwa inatisha. katika muda mfupi, lilitokea shimo katika uwanja. shambulio lilikuwa baya sana " Olena aliniambia.

Valerii na Olena walitishwa na mashambulio

"Nimeishi maisha yangu yote hapa. Nilikwenda shule hapa. Nilisafisha bustani, nilipanda majani. Mwanangu wa kiume na sasa mjukuu wangu walikulia hapa," alisema mume wake Valerii. "Kila wakati kumekuwa na watoto wengi hapa. "Ninadhani walitaka kupiga jengo la chuo kikuu na mnara wa Hrushevsky.

Hizo ni alama muhimu kwetu sisi , lilikuwa ni shambulio la maeneo muhimu." Mashambulio yaliyolenga maeneo muhimu? Ni vigumu, mapema hivi, ni vigumu kutambua mantiki yake.

Lakini ripoti kutoka maeneo mengine zinazungumzia kushambuliwa kwa mtambo wa nishati wa kuchemsha maji katika eneo la Lviv. Rais Volodymyr Zelensky anasema maeneo ya nishati yanashambuliwa kote nchini.

Ni muda mrefu tangu miji mini ishambuliwe kwa wakati mmoja. Moscow kwa sasa imeazimia kutuma ujumbe mkubwa kadri iwezekanavyo.

Siku mbili zilizopita, mitandao ya kijamii ilifurika video na memes zinazoonyesha Waukraine wakisherehekea shambulio kwenye daraja linaloiunganisha nchi hiyo na rasi ya Crimea.

Leo, video zote zinaonyesha wakazi walioshitushwa na mashambulio ya makombora, vifusi vya moto na tahadhari za dharura. Hisia yoyote ya furaha imetoweka.

Kuna hisia kwamba mashambulio hayaepukiki, lakini hilo halipunguzi mshituko. Hofu kwa mara nyingine imeukumba mji mkuu.

View Comments