Image: BBC

Rais wa Tanzania Samia Suluhu ametoa ametoa pole kwa kwa wafiwa na majeruhi wa ajali ya ndege iliyotokea Jumapili huko Bukoba,Kagera .

Watu 19 walifariki katik ajali hiyo na wengine 26 kuokolewa .

Katika ujumbe wake wa pole,rais Samia pia amewashukuru wakazi wa Kagera kwa ujasiri,ushirikiano na jitihada walizofanya kuwaokoa abiria waliozama na ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba kupitia Mwanza.

Precision Air ndiyo shirika kubwa la ndege la kibinafsi la Tanzania na kwa kiasi fulani inamilikiwa na Kenya Airways. Ilianzishwa mnamo 1993 na inaendesha safari za ndege za ndani na kikanda.

View Comments