In Summary

• Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine ilifunguliwa siku ya Jumanne wakati Urusi ilipozindua mashambulizi yake makubwa zaidi ya makombora katika muda wa miezi tisa.

BBC

Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg ameiambia BBC kwamba kombora lililoua watu wawili nchini Poland siku ya Jumanne huenda lilikuwa la Ukraine.

"Uwezekano mkubwa hili ni kombora la ulinzi wa anga la Ukraine," alisema huku uchunguzi ukiendelea kuhusu mlipuko huo karibu na mpaka wa Ukraine.

Lakini alisisitiza kuwa Urusi ndio inayoweza kulaumiwa kwa sababu ya uvamizi wake unaoendelea Ukraine.Ukraine yenyewe inaendelea kusema kuwa Urusi ndio ilirusha kombora hilo na si wao."Sina shaka kuwa hili sio kombora letu," Rais Volodymyr Zelensky alisema katika hotuba yake kwenye televisheni.

"Ninaamini kuwa hili lilikuwa kombora la Urusi, kulingana na ripoti zetu za kijeshi."Alisema ilikuwa muhimu kwa Ukraine kuruhusiwa kujiunga na uchunguzi wa mlipuko kwenye shamba la Przewodow, kilomita 6 (maili 4) kutoka mpakani.

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine ilifunguliwa siku ya Jumanne wakati Urusi ilipozindua mashambulizi yake makubwa zaidi ya makombora katika muda wa miezi tisa tangu uvamizi huo wa tarehe 24 Februari.Makumi ya makombora ya Urusi yalilenga nchi hiyo lakini Ukraine inasema ilifanikiwa kudungua mengi kati yao.Shambulio hilo, lililotokea wakati wa mkutano wa G20 nchini Indonesia, lilisababisha kilio cha kimataifa, huku habari za mlipuko wa kombora ndani ya eneo la Poland mwanachama wa Nato zikizusha hofu kwamba huenda vita hivyo vikiongezeka kwa hatari.

Bw Stoltenberg alisema Nato iliahidi kutoa"mfumo wa hali ya juu zaidi wa ulinzi wa anga" kwa Ukraine ambayo si mwanachama wa muungano huo lakini inapokea msaada mkubwa wa kijeshi.

"Leo nilihudhuria mkutano wa kikundi cha usaidizi cha Ukraine ambapo washirika wa Nato na washirika walitoa ahadi mpya kwa mifumo ya juu zaidi ya ulinzi wa anga ili tuweze kusaidia kuangusha makombora ya Urusi," mkuu wa Nato alisema."Lakini njia bora ya kuzuia matukio kama haya katika siku zijazo ni kwa Urusi kuacha vita."

"Hatuna dalili kwamba hili ni shambulio la makusudi kutoka Urusi," alisema, akizungumza kutoka makao makuu ya Nato huko Brussels.

Aliongeza, hata hivyo, kwamba "hakuna shaka kwamba Urusi inahusika kwa sababu hili lisingetokea ikiwa Urusi haingeanzisha mashambulizi ya makombora dhidi ya miji ya Ukraine jana, kama wamefanya mara nyingi kabla wakati wa vita hivi".

Rais wa Poland Andrzej Duda alisema hapo awali kwamba ingawa kombora la S-300 lililotengenezwa na Urusi ndilo lenye uwezekano mkubwa wa kulaumiwa, hakuna ushahidi kwamba lilirushwa na upande wa Urusi.

View Comments