In Summary

• Katika picha ambazo zilisambazwa mitandaoni, watu wanaonekana wakiwashambulia mbwa hao kwa mawe kabla ya kuwamwagia mafuta na kuwachoma moto.

Mbwa wa kurandaranda mitaani,
Image: Getty Images, Soweto Live

Mbwa watatu wa kuradnaranda mitaani walipigwa mawe hadi ufa kabla ya kuteketezwa kwa moto baada ya kumvamia mtoto msichana wa shule.

Tukio hili ambalo lilitokea nchini Afrika Kusini katika mji wa Cape Town limezua gumzo kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii haswa baada ya adhabu hiyo ambayo haijawahi kutokea kwa wanyama aina ya mbwa.

Katika picha ambazo zilisambazwa mitandaoni, watu wanaonekana wakiwashambulia mbwa hao kwa mawe kabla ya kuwamwagia mafuta na kuwachoma moto hadi kuwa majivu.

“Mbwa walikuwa wamemvamia msichana mdogo katika uwanja wa Gatesville. Mtoto alipata majeraha mabaya na kulazimika kukimbizwa katika hospitali iliyo karibu kwa matibabu,” kilisema Chama cha Kuzuia Ukatili kwa Wanyama (SPCA) cha Cape of Good Hope kulingana na nukuu katika vyombo vya habari nchini humo.

"Jamii ilichukua hatua mikononi mwao na kuwashambulia mbwa hao, kuwapiga mawe, kuwachoma visu na kuwapiga wanyama hao kwa vitu kabla ya kuwachoma hadi kufa."

Tukio hili linajiri huku mamlaka nchini humo ikianzisha mchakato wa kuwaweka vizuizi salama wanyama wote haswa mbwa ambao wanarandaranda mitaani kutoka jalala moja kuelekea lingine kwa ajili ya kusasambua mapipa ya taka.

Mkurugenzi wa Chama hicho cha kuzuia ukatili kwa wanyama aidha alionya hatua hiyo ya wananchi wenye ghadhabu kuchukua sheria mikononi na kuwashambulia wanyama na kusema kuwa haifai hivyo kwani kuna sehemu husika za kupiga ripoti ili kuhakikisha wanyama hao wanaondolewa sehemu za kuhatarisha maisha ya watu.

Aliwataka wenye wanyama kama hao wa kuranda hovyo mitaani kuwajibika na kama mtu una boma lenye usalama wa kutosha basi haina haja kufuga wanyama hao ambao baadae hugeuka kero na kuzua athari kwa watu wanaoishi karibu na boma lako.

“Inasikitisha mtoto alijeruhiwa na wanyama walishambuliwa kikatili. Hakuna mbwa anayepaswa kuzurura mitaani. Wamiliki wa wanyama-vipenzi wanaowajibika huhakikisha wanyama wao wanahifadhiwa ndani ya mali zao. Ikiwa nyumba yako haina uzio wa kutosha, usipate mbwa. Tunawahimiza umma kuwasiliana na SPCA ikiwa mbwa ana tabia ya fujo au anajaribu kumng'ata mtu. Tutachukua mbwa mara moja. Watu hawapaswi kuchukua mambo mikononi mwao. Hakuna mnyama anayestahili kuvumilia ukatili na mateso.”

View Comments