In Summary
  • Rais wa sasa President Félix Tshisekedi, ambaye aliingia kwa mara ya kwanza madarakani Januari 2019, tayari amekwishasema atagombea tena muhula wa pili, kulingana na AFP

Uchaguzi wa urais katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo utafanyika tarehe 20 Disemba mwaka ujao ,tume ya uchaguzi imetangaza.

Kwa sasa, hali ya usalama inayoyakumba maeneo ya mashariki mwa nchi huku waasi mbali mbali wakisababisha ukosefu wa usalama.

Jaribio la kulitaka kundi la waasi wa M23 kusitisha mapigano lilionekana kugonga mwamba.

Shirika la habari AFP linaripoti kuwa tume ya uchaguzi imekiri kuwa "kuna ukosefu wa usalama unaoendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi " ambao unaweza kuzuiwa kufanyika kwa uchaguzi "huru, wa kidemokrasia na wa uwazi’’ unaoweza kuwa changamoto kwa shughuli ya upigaji kura.

Lakini maafisa wameazimia kuzingatia ratiba.

"Sio suala la majadiliano kuhusu ukomo uliowekwa na katiba, ni swala la sisi kuheshimu katiba na demokrasia yetu ," msemaji wa serikali Patrick Muyaya amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema.

Anakadiria kuwa uchaguzi utagarimu karibu dola milioni 600, Reuters imeripoti.

Rais wa sasa President Félix Tshisekedi, ambaye aliingia kwa mara ya kwanza madarakani Januari 2019, tayari amekwishasema atagombea tena muhula wa pili, kulingana na AFP.

Alichukua mamlaka kutoka kwa Joseph Kabila – ambapo ilikuwa na mara ya kwanza kwa marais wa Congo kukabidhiana mamlaka kwa amani.

 

 

 

 

View Comments