In Summary

•Omar Bin Laden amethibitisha kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo baba yake alitekeleza lakini yeye binafsi hayakumfurahisha.

•Osama bin Laden aliuawa katika operesheni iliofanywa na wanajeshi wa Marekani huko Abbottabad, Pakistan.

Osama bin laden na al -Zawahiri
Image: BBC

Omar Bin Laden mtoto wa Osama Bin Laden ametoa taarifa za kushangaza kumhusu baba yake.

Omar Bin Laden amezungumza na gazeti la The Sun, na kuthibitisha kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo baba yake alitekeleza lakini yeye binafsi hayakumfurahisha.

Miongoni mwayo ni pamoja na kusema kuwa baba yake alifuga mbwa ambao Kiislamu huchukuliwa kama uchafu.

Mke wa kwanza wa Osama Bin Laden, Najvi Bin Laden, alimwambia Jean Sassoon katika kitabu chake kwamba,

"Mume wangu Osama Bin Laden aliagiza mbwa wawili kutoka Ulaya ambao ni Safir na Zair.

"Nilishangaa Omar aliponiambia kuwa baba yake huko Khartoum alikuwa akifuga mbwa kwa sababu Waislamu na mbwa ni kama moto na mafuta".

Najvi aliongeza kuwa mmoja wa mbwa hao aliibwa huku mwingine akiugua na kufa.

Miaka saba baada ya kitabu hicho kuchapishwa, mtoto wa Osama Bin Laden, Omar Bin Laden, ambaye alifanya mahojiano na gazeti la The Sun, alisema kuwa babake Osama Bin Laden alifanyia majaribio mbwa wake silaha za kemikali.

Osama bin Laden aliuawa katika operesheni iliofanywa na wanajeshi wa Marekani huko Abbottabad, Pakistan.

"Niliona (vipimo vya silaha za kemikali vikifanyiwa mbwa, sikufurahia jambo hilo," alisema Omar Bin Laden.

"Nilijaribu kusahau kumbukumbu hizo zote mbaya kuhusu tukio hilo.

"Ni vigumu lakini baada ya muda, utasahau."

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Omar bin Laden kwenda Afghanistan kukutana na baba yake na familia yake. Familia hiyo ilikuwa na mbwa aliyeitwa "Bobby".

Wanafunzwa kuwa mbwa walinzi wanaosaidia usalama kulingana na Omar Bin Laden.

Kitabu kilichoandikwa kuhusu Osama Bin Laden kinasema kwamba mbwa huyo alikufa ghafla.

Lakini hakuna anayejua kwa nini alikufa.

Omar Bin Laden ni nani?

Omar bin Laden sasa ana umri wa miaka 41.

Aliishi Sudan na baba yake Osama Bin Laden kuanzia mwaka 1991 hadi 1996.

Baada ya kutengana kwa Omar na baba yake, alikiri kwamba alipata mafunzo ya matumizi ya silaha katika kambi za mafunzo za al-Qaeda.

Omar alisema katika kitabu hiki kwamba haikubaliki kwa baba yake kuua raia, na ndiyo maana aliondoka Al-Qaeda, aliongeza.

Hata hivyo, baba yangu hakufurahishwa na uamuzi huu".

Omar kisha akarudi Saudi Arabia na kuanza biashara mwaka 2006 na baadaye anakaenda Ulaya.

Umar aliwahi kuoa lakini baadaye alitengana na mke wake ambaye alipata mtoto wa kiume.

Omar alisema nini kuhusu baba yake Osama Bin Laden?

Katika mahojiano na gazeti la The Sun, Omar alisema, Mnamo Mei 2, 2011, nilikuwa Qatar ilipogundulika kuwa Jeshi la Wanamaji la Marekani lilimuua baba yangu katika mji mmoja nchini Pakistan.

Hata hivyo, Omar haamini kuwa Marekani ilizika mwili wa babake Osama bin Laden baharini.

View Comments