Kila sekunde iendayo kwa Mungu, maajabu na matukio yasiyo ya kawaida huripotiwa katika sehemu mbali mbali duniani.
Tukio moja la sampuli hiyo limeripotiw nchini Marekani ambapo mbwa amemuua mtu kwa kumpiga risasi.
Kulingana na jarida la AFP, mbwa huyo alikanyaga kwa bahati mbaya bunduki iliyokuwa imewekwa katika kiti cha nyuma cha gari aina ya pick-up.
Mguu wa mbwa huyo ulikanyaga kitufe cha kufyatua risasi, ambalo lilimpata mtu mwenye alikuwa ameketi katika kiti cha mbele kando ya dereva na kumuua papo hapo.
Tukio hilo lilitokea katika Jimbo la Kansas na polisi walisema kuwa mwenye mbwa huyo na mwa wake walikuwa wametoka ili kufanya uwindaji kiasi.
"Mbwa wa mmiliki wa gari hilo alikanyaga bunduki, na kusababisha silaha kutolewa. Duru ya risasi ilimpiga abiria, ambaye alikufa kutokana na majeraha yake kwenye eneo la tukio," ofisi ya Sherifu wa Kaunti ya Sumner ilinukuliwa na jarida hilo.
"Uchunguzi unaendelea, lakini uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ni ajali inayohusiana na uwindaji," ofisi ya sheriff iliongeza katika taarifa tofauti.
Maafisa hawakusema iwapo mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 30 aliyefariki alikuwa mmiliki wa mbwa huyo.
Ufyatuaji risasi wa ajali ni jambo la kusikitisha sana nchini Marekani, nchi ambayo kuna bunduki nyingi kuliko watu. Kulingana na data kutoka kwa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Merika, zaidi ya watu 500 walikufa katika ajali za bunduki mnamo 2021.