In Summary
  • Kwa kusitisha uchumba wao baada ya miaka minne, Hakimu Asanasio Mukobi aliamua kuwa Bi Kyarikunda alikiuka ahadi na kusababisha madhara kwa Tumwine
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Mwanamke mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba wake ameamrishwa na mahakama kulipia hasara za kifedha kwa uchungu wa kisaikolojia.

Mahakama ya Kanungu ilisema kuwa Richard Tumwine alilipa shilingi milioni 9.4($2,550; £2,060) kwa ajili ya masomo ya sheria ya Bi Fortunate Kyarikunda, pesa ambazo sasa atatakiwa kuzilipa pamoja na gharama za kesi.

Kwa kusitisha uchumba wao baada ya miaka minne, Hakimu Asanasio Mukobi aliamua kuwa Bi Kyarikunda alikiuka ahadi na kusababisha madhara kwa Tumwine.

Mahakama ilisema kuwani "isiyo na maana, upotoshaji na ulaghai" kwa mshitakiwa kudai kuwa wazazi wake walimwambia asiolewe na mwanaume mzee sana, ikisema" alikuwa na wakati wote wa kukataa maombi ya mapenzi mapema na kuepuka kutumia pesa zake ".

Haijulikani iwapo Bi Kyarikunda atakata rufaa dhidi ya hukumu.

Wakosoaji wanasema gazeti la Monitor kwamba hukumu ina kasoro kwasababu uchumba ni tofauti na ndoa ambayo inakubalika kisheria.

Wakati huo huo Sheila Kawamara, kutoka kikundi cha utetezi wa wanawake ED EASSI, anaonye kuwa wakati mwingine huwa kuna hali za unyonyaji ambapo mwanaume humpatia pesa mwanamke kwa sharti kuwa atamuoa.

 

 

 

View Comments