In Summary

• Mahakama ilisema kuwa mwanzo atatumikia miaka 30 jela bila rufaa yoyote kabla ya mmsamaha kuanza kuzingatiwa.

Mfungwa akiwa jela
Image: Mfungwa Jela

Afisa mmoja wa polisi alijizolea kibano cha maisha gerezaji kwa kupatikana na hatia ya kutumia cheo chake kuwabaka wanawake 12.

Jarida la AFP liliripoti kwamba afisa huyo wa jiji la London nchini Uingereza alihukumiwa vifungo 36 vya maisha, huku kifungo cha chini kikiwa cha miaka 30 kwa msururu wa visa 71 vilivyotuhimiwa dhidi yake kwa kuwabaka wanawake 12.

Jaji alisema kuwa afisa huyo wa polisi ambaye uhalifu wake ulijumuisha visa vya ubakaji 48, uliwakilisha "hatari kubwa kwa wanawake" ambayo "itadumu kwa muda usiojulikana".

Afisa huyo kwa jina Carrick, mwenye miaka 48, afisa wa muda mrefu wa kitngo cha Metropolitan, jeshi kubwa la polisi la Uingereza, atatumikia miongo mitatu gerezani kabla ya kuzingatiwa kwa msamaha.

Kitengo cha Metropolitan wameapa kukomesha utamaduni wa chuki dhidi ya wanawake na uzembe ulioangaziwa na ubakaji na mauaji ya msichana ambaye alinyakuliwa barabarani na afisa wa polisi mnamo Machi 2021.

Tuhuma za ubakaji kutoka kwa maafisa wa polisi nchini Uingereza si jambo geni kuripotiwa, jambo ambalo limechafua picha na heshima ya maafisa wa polisi katika taifa hilo la Kikoloni.

Nchini Uingereza kwa sasa imekumbwa na msukosuko mkubwa wa kiuchumi, mamia ya watu wakijitosa kwenye barabara wakiandamana kwa kile wanakitaja kama ugumu wa gharama ya maisha.

Maandamano hayo ambayo yalianza wiki jana yameshuhudia shughuli mbali mbali zikilemazwa, miezi michache tu baada ya waziri mkuu Rishi Sunak kuchukua hatamu kutoka kwa waziri mkuu wa muda mfupi aliyeteuliwa na marehemu malkia Elizabeth wa pili, Liz Truss.

View Comments