In Summary

• Mnamo Machi 27, 2020, papa aliwahimiza wafuasi ambao walihisi "kuogopa na kupotea" mbele ya kile ambacho wakati huo kilikuwa virusi vya kutisha kuwa na imani.

Katoliki kutuma ujumbe wa matumaini wa papa mwezini
Image: Catholic News

Makao makuu ya kanisa katoliki kule Vatican, Italai wametangaza mpango wa kutuma ujumbe wa matumaini wa papa Francis kwenda angani.

Ujumbe huo wa Papa Francis ni ule ambao alionekana akifanya maombi akiwa peke yake katika ukumbi wa Mtakatifu Petro katikati mwa janga la Covid-19 mwaka 2020.

Hotuba ya papa akiomba peke yake katika uwanja tupu wa St Peter's imegeuzwa kuwa "kitabu cha nano" chenye upana wa chini ya milimita mbili, ambacho kitazinduliwa na kutumwa mwezini mnamo 10 Juni.

Itasafiri kuzunguka Dunia kwa satelaiti iliyoundwa kimakusudi katika mwinuko wa takriban kilomita 525, ikitumwa kwa roketi ya SpaceX Falcon 9 kutoka Vandenberg Space Force Base huko California, AFP waliripoti.

Mradi wa "Spei Satellites" (Satellites of Hope katika lugha ya Latin) -- ambao gharama na ufadhili wake haujafichuliwa -- unaratibiwa na Shirika la Anga la Italia kwa ushirikiano na taasisi mbalimbali za Italia.

Mnamo Machi 27, 2020, papa aliwahimiza wafuasi ambao walihisi "kuogopa na kupotea" mbele ya kile ambacho wakati huo kilikuwa virusi vya kutisha kuwa na imani.

Mradi huo sio wa kwanza kwa papa kukutana na anga -- mwaka wa 2017, alipiga simu ya video na wanaanga kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga cha Juu (ISS), ambapo aliwauliza kuhusu "mahali pa mwanadamu katika ulimwengu".

Miaka sita mapema, mtangulizi wake Benedict XVI pia alipigia ISS.

View Comments