In Summary

•Kumekuwa na wimbi la hukumu ya kunyongwa katika Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran, jambo lililoibua maandamano ndani na nje ya Iran.

•Kikundi cha kutetea haki za binadamu kimeita hukumu za vifo "kitendo cha ukatili cha utawala wa kale".

Image: BBC

Iran imewanyonga wanaume wawili waliopatikana na hatia ya "kuchoma Quran" na "kumtusi Mtume wa Uislamu", imesema mahakama ya nchi hiyo.

Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli-Zare walikuwa wakimiliki makumi ya akaunti za mitandao ya kijamii "kwa ajili ya watu wanaomkana Mungu nakukiuka maadili ya kidini ", liliripoti shirika la habari la mahakama ,Mizan.

Wakili wa Bw Mehdad alikuwa amesisistiza kuwa hakuwa na hatia na kwamba hukumu yake sio ya haki.

Kikundi cha kutetea haki za binadamu kimeita hukumu za vifo "kitendo cha ukatili cha utawala wa kale".

Kumekuwa na wimbi la mauaji ya kunyonga katika Jamuhuri hiyo ya Kiislamu, huku ghasia za upinzani dhidi ya serikali zikiendelea, lakini mauaji hayo ni nadra kwa waliopatikana na hatia ya kukufuru.

Mizan lilisema kuwa Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli-Zare walinyongwa katika gereza la Arak Prison lililopo kati katiimwa Iran Jumatatu asubuhi.

Wanaume hao wawili walikuwa wamekamatwa mwaka 2020 na kushitakiwa kwa kuendelesha kituo cha Telegram kinachoitwa "Ukosoaji wa imani za kufikirika na dini ", kulingana na Shirika la wanaharakati wa haki za binadamu la Iran (HRANA).

View Comments