logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ajali ya boti Ugiriki yasababisha vifo vya watu 79 huku mamia wakipotea

Boti hiyo ilisafiri takriban kilomita 80 kusini-magharibi mwa Pylos, baada ya kukataa msaada.

image
na Davis Ojiambo

Habari15 June 2023 - 08:25

Muhtasari


  • • Walinzi wa pwani walisema mashua hiyo ilionekana katika maji ya kimataifa Jumanne jioni na ndege ya shirika mpakani la EU Frontex.
Walinzi wa pwani wa Ugiriki walitoa picha za mashua hiyo iliyojaa watu kabla haijazama.

Takriban watu 79 wamefariki na wengine zaidi ya 100 kuokolewa baada ya meli yao ya uvuvi kuzama katika pwani ya kusini mwa Ugiriki.

Lakini walionusuriwa na maafisa wa Ugiriki wanasema kuwa mamia zaidi ya wahamiaji walikuwa ndani ya boti hiyo.

Serikali inasema hili ni mojawapo ya majanga makubwa zaidi ya wahamiaji Ugiriki, na imetangaza siku tatu za maombolezo.

Boti hiyo ilisafiri takriban kilomita 80 (maili 50) kusini-magharibi mwa Pylos baada ya walinzi wa pwani kusema kuwa imekataa msaada.

Walinzi wa pwani walisema mashua hiyo ilionekana katika maji ya kimataifa Jumanne jioni na ndege ya shirika mpakani la EU Frontex.

Hakuna mtu kwenye boti ambaye alikuwa amevaa jaketi za kuokoa maisha, iliongeza.

Ikinukuu mifumo ya uendeshaji na wizara ya meli, shirika la utangazaji la Ugiriki ERT lilisema mamlaka ilifanya mawasiliano na boti hiyo kupitia simu ya satelaiti mara kadhaa na kutoa msaada, lakini waliambiwa mara kwa mara: "Hatutaki chochote zaidi ya kwenda Italia."

Saa chache baadaye, karibu 01:00 (23:00 GMT), mtu kwenye mashua aliripotiwa kuwajulisha walinzi wa pwani wa Ugiriki kwamba injini ya meli ilikuwa na hitilafu.

Muda mfupi baadaye, boti ilipinduka, na kuchukua dakika kumi hadi kumi na tano tu kuzama kabisa.

Operesheni ya utafutaji na uokoaji ilianzishwa lakini ilitatizwa na upepo mkali.

Simu yenye nambari ya usaidizi wa dharura kwa wahamiaji walio katika matatizo baharini inasemekana ilitoa tahadhari, walinzi wa pwani "walikuwa wakifahamu meli hiyo kuwa katika taabu kwa saa kadhaa kabla ya msaada wowote kutumwa", na kuongeza kuwa mamlaka "imearifiwa na vyanzo tofauti" kwamba mashua ilikuwa na matatizo.

Iliongeza kuwa watu hao inawezekana walikuwa na hofu ya kukutana na mamlaka ya Ugiriki kwa sababu walikuwa wanafahamu "tabia zisizofaa na mwitikio mbaya ambao wangepata".

Boti hiyo inakisiwa kuwa ilikuwa ikitoka Libya kuelekea Italia, huku wengi wa waliokuwemo wakiaminika kuwa wanaume wenye umri wa miaka 20.

Walikuwa wakisafiri kwa siku nyingi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani, ambazo ziliongeza kuwa mashua hiyo ilifikiwa na meli ya mizigo ya Malta Jumanne alasiri ambayo ilitoa chakula na maji.

Walionusurika walisema kulikuwa na kati ya watu 500 hadi 700 kwenye bodi na mkurugenzi wa afya wa mkoa Yiannis Karvelis alionya juu ya janga ambalo halijawahi kutokea: "Idadi ya watu waliokuwemo ilikuwa kubwa zaidi kuliko uwezo ambao unapaswa kuruhusiwa kwa mashua hii."

Mlinzi wa Pwani Cpt Nikolaos Alexiou aliiambia TV ya umma kwamba wenzake walikuwa wameona watu wakiwa wamejazana kwenye sitaha na kwamba mashua ilikuwa imezama katika sehemu moja ya kina kabisa ya Mediterania.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved