In Summary

• Benedict alifariki mwezi Desemba akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kudhoofika kwa muda mrefu kiafya.

• Alikuwa mtakatifu wa kwanza kufanya uamuzi wa kuachia ngazi mamlaka kama Papa kwa zaidi ya miaka 600 iliyopita.

Papa Benedict 16
Image: BBC News

Msalaba ambao papa wa zamani Benedict wa 16 aliuvaa kifuani umeibwa kutoka kwa kanisa moja kusini mwa Ujerumani ambako ulikokuwa umewekwa kama maonyesho, polisi walisema Jumanne kama ilivyoripotiwa na jarida la AFP.

Msalaba wa kifuani ulikuwa katika boksi katika ukuta wa kanisa la Mtakatifu Oswald huko Traunstein, katika jimbo la Bavaria, ambapo marehemu Benedict alitumia miaka yake ya ujana.

Wezi waliingilia boksi hilo na kuchukua bidhaa hiyo, ambayo papa wa zamani alikuwa ameiachia parokia hiyo, kati ya 11:45 am na 5:00 pm siku ya Jumatatu.

"Kwa Kanisa Katoliki, thamani ya kitu hiki kitakatifu haiwezi kuhesabiwa," polisi wa Bavaria walisema katika taarifa iliyonukuliwa na AFP.

Wahalifu hao ambao majina yao hayajafahamika, pia walivamia daftari la kuhifadhia fedha la stendi ya magazeti na kuiba fedha hizo zilizokuwa ndani, polisi walisema.

Wanaomba mashahidi ambao wanaweza kuwa wamemwona mtu yeyote akitenda kwa mashaka karibu na kanisa siku ya Jumatatu.

Benedict, ambaye mwaka 2013 alikuwa papa wa kwanza katika kipindi cha karne sita kujiuzulu kama mkuu wa Kanisa Katoliki, alifariki mwezi Desemba akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kudhoofika kwa muda mrefu kiafya.

Alikuwa mtakatifu wa kwanza kufanya uamuzi wa kuachia ngazi mamlaka kama Papa kwa zaidi ya miaka 600 iliyopita.

Kinyume na Benedicto wa 16 ambaye alikuwa na misimamo mikali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, mrithi wake Papa Francisco katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akinukuliwa kwa njia mbalimbali akionekana kukaribisha suala la mapenzi ya jinsia moja katika kanisa.

Alichaguliwa kuwa papa mnamo Aprili 2005, kufuatia kifo cha John Paul II.

Alijulikana kuwa na msimamo mkali zaidi kuliko mrithi wake, Papa Francis, ambaye alichukua hatua za kupunguza msimamo wa Vatican juu ya uavyaji mimba na ushoga, pamoja na kufanya zaidi kukabiliana na janga la unyanyasaji wa kijinsia ambalo limelikumba kanisa hilo katika miaka ya hivi karibuni na kugunduliwa. 

 

View Comments