In Summary

• Kwa mujibu wa arifa ya ndani ya serikali ya Marekani iliyoonekana na vyombo vya habari vya Marekani, sauti hizo zilisikika na ndege kila baada ya muda wa dakika 30 siku ya Jumanne.

Image: BBC

Waokoaji waliokuwa wakitafuta sehemu ya chini ya maji ya chombo cha watalii kilichopotea karibu na eneo la ajali ya Titanic wameripotiwa kusikia sauti za kishindo karibu na eneo ambalo nyambizi hiyo ndogo hiyo ilipotea.

Kwa mujibu wa arifa ya ndani ya serikali ya Marekani iliyoonekana na vyombo vya habari vya Marekani, sauti hizo zilisikika na ndege kila baada ya muda wa dakika 30 siku ya Jumanne.

Sona ya ziada ilitumiwa saa nne baadaye na sauti hizo bado zilisikika.

BBC imewasiliana na Idara ya Usalama wa Taifa na Walinzi wa Pwani kwa maoni.

CNN na Rolling Stone zote zililiripoti juu ya hatua hiyo.

Watu watano walikuwa kwenye chombo hicho wakati mawasiliano yalipopotea saa moja na dakika 45 ndani ya kuanza safari yake siku ya jumapili.

Kulingana na Walinzi wa Pwani ya Marekani , watu hao wana chini ya masaa 30 ya oksijeni iliyobaki.

Operesheni ya utafutaji katika jimbo la Newfoundland nchini Canada hadi sasa imeshindwa kupata chochote.

Hata hivyo, imeongezwa kwa upana ili kujumuisha rasilimali zaidi na utaalamu wa uokoaji kutoka kwa makampuni binafsi.

View Comments