In Summary

• "Mawasiliano yao yalipotea, na urambazaji pia ulipotea - na nikasema papo hapo, huwezi kupoteza mawasiliano na urambazaji kwa pamoja bila tukio la janga kubwa."

Mwongoza filamu wa Hollywood James Cameron, ambaye aliongoza filamu ya Titanic ya mwaka 1997.
Image: BBC

Mwongoza filamu wa Hollywood James Cameron, ambaye aliongoza filamu ya Titanic ya mwaka 1997, ameiambia BBC kuwa alihisi hadi kwenye mifupa yake tukio la kupotea kwa nyambizi ya Titan na hatimaye kuzama kwenye bahari.

Cameron amesafiri mara 33 hadi mwenye eneo la ajali ya Titanic.

Alisema alikuwa kwenye meli siku ya Jumapili wakati nyambizi ya Titan ilipopotea, na hakusikia juu yake hadi Jumatatu.

Alipopata taarifa kwamba nyambizi hiyo ilikuwa imepoteza mawasiliano, alisema alishuku janga huenda limetokea.

"Nilihisi katika mifupa yangu kile kilichotokea. Ukipoteza umeme kwenye nyambizi na mfumo wake wa mawasiliano pia haupatikani – basi nyambizi hiyo imetoweka."

Mwelekezaji huyo aliendelea: "Bila kupoteza wakati nilipiga simu kwa baadhi ya wandani wangu katika jumuiya ya nyambizi. Ndani ya saa moja nilikuwa na ujumbe ufuatao. Walikuwa kwenye mteremko. Walikuwa katika mita 3500, wakielekea chini kwa mita 3800.

"Mawasiliano yao yalipotea, na urambazaji pia ulipotea - na nikasema papo hapo, huwezi kupoteza mawasiliano na urambazaji kwa pamoja bila tukio la janga kubwa. Na jambo la kwanza ambalo lilinijia akilini lilikuwa ni kulipuka. "

Siku ya Alhamisi, afisa kutoka Jeshi la Wanamaji la Marekani aliambia mshirika wa BBC CBS News kwamba jeshi la wanamaji liligundua "sauti inayoendana na milipuko" muda mfupi baada ya Titan kupoteza mawasiliano.

Afisa huyo alisema taarifa hizo ziliwasilishwa kwa timu ya Walinzi wa Pwani ya Marekani ambayo iliitumia kupunguza eneo la utafutaji.

Cameron aliiambia BBC wiki iliyopita "alihisi kama tukio la muda mrefu na la kutisha ambapo watu wanakimbia huku na huko wakizungumza kuhusu kelele za kugonga na kuzungumza juu ya oksijeni na mambo haya mengine yote".

"Nilijua kuwa nyambizi hiyo ilikuwa imefika chini kina cha mwisho. Hapo ndipo walipoipata," aliendelea.

Aliongeza kuwa mara kifaa cha chini ya maji kinachoelekezwa ilipotumwa siku ya Alhamisi, watafiti "waliipata ndani ya saa, labda ndani ya dakika".

View Comments