In Summary

• Waliokuwa katitka nyambizi hiyo ni pamoja na Stockton Rush, Mkurugenzi Mtendaji wa OceanGate Shahzada Dawood, 48, mtoto wake Suleman, 19, na mfanyabiashara wa Uingereza Hamish Harding, 58.

Image: DAWOOD FAMILY/LOTUS EYE PHOTOGRAPHY

Watu watano waliokufa kwenye nyambizi ya Titan chini ya maji walikuwa "wagunduzi wa kweli", kampuni iliyoendesha shughuli za kutalii eneo la ajali ya meli ya Titanic imesema .

Wanaume hao "walishiriki moyo wa pamoja ya ugunduzi ," OceanGate ilisema katika taarifa,

Wanaume hao watano walikufa katika kile walinzi wa Pwani wanaamini kuwa ni janga kubwa.

Ilisema kuwa vifusi viligunduliwa karibu na eneo la ajali ya Titanic mapema Alhamisi asubuhi.

Meli hiyo ilitoweka siku ya Jumapili.

Wanaume waliokuwa kwenye nyambizi hiyo ndogo ni pamoja na Stockton Rush, Mkurugenzi Mtendaji wa OceanGate mwenye umri wa miaka 61, pamoja na mfanyabiashara wa Uingereza-Pakistani Shahzada Dawood, 48, mtoto wake Suleman, 19, na mfanyabiashara wa Uingereza Hamish Harding, 58.

Mwanaume wa tano kwenye nyambizi hiyo, Paul-Henry Nargeolet, alikuwa mpiga mbizi wa zamani wa jeshi la wanamaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 77 na mpelelezi mashuhuri.

Katika mkutano na wanahabari siku ya Alhamisi, Admirali John Mauger wa Walinzi wa Pwani ya Marekani alisema kuwa mabaki hayo yanaaminika kuwa sawa na nyambizi ya Titan.

Haijulikani ni nini kilisababisha uharibifu wa Titan.

Kutoweka kwa nyambizi hiyo kulisababisha juhudi kubwa ya utafutaji wa kimataifa iliyohusisha vikosi vya Marekani, Kanada, Uingereza na Ufaransa.

Katika taarifa, OceanGate ilisema inathamini "kujitolea kwao kutafuta wavumbuzi hawa watano, mchana na usiku wao wa kufanya kazi bila kuchoka kusaidia wafanyakazi wetu na familia zao".

Mabaki hayo yalipatikana na gari la utafutaji la chini ya maji linalodhibitiwa kwa mbali (ROV) takriban futi 1,600 (480m) kutoka kwenye mabaki ya Titanic.

Vipande vitano tofauti viligunduliwa ambavyo viliruhusu mamlaka kuthibitisha kuwa vilitoka kwa Titan, ikiwa ni pamoja na sehemu ya mkia.

Haijulikani ni lini hitilafu hiyo ilitokea au ni nini huenda kilisababisha.

Adm Mauger alisema hakuwa na jibu la iwapo miili ya watu hao watano waliokuwemo kwenye nyambizi inaweza kupatikana.

"Haya ni mazingira ya ajabu yasiyosameheka huko chini kwenye sakafu ya bahari," alisema.

ROV's zitasalia katika eneo hilo huku uchunguzi wa kilichotokea ukiendelea, Mauger aliongeza.

Wafanyakazi wengine - ikiwa ni pamoja na wataalam wa matibabu na mafundi - wataanza kuondoka.

Mapema wiki hii, mamlaka ilisema kwamba ndege za Canada ziligundua sauti za chini ya maji, ambazo baadhi ya wataalam walikisia kuwa huenda zilikuwa ishara kwamba abiria nyambizi hiyo walikuwa bado hai.

Walinzi wa Pwani sasa wanaamini kuwa hakukuwa na uhusiano kati ya kelele na eneo ambalo mabaki ya Titan yalipatikana kwenye sakafu ya bahari.

Hatua zinazofuata

Image: REUTERS

Walinzi wa Pwani wa Marekani wanasema mawazo yao yapo na familia na kuhakikisha wanaelewa vizuri kadiri wanavyoweza kuhusu kile kilichotokea na kuanza kukubali kilichotokea kwa wapendwa wao.

Kwa upande wa mchakato huo mkubwa, wataendelea kuchunguza eneo la bahari ambako mabaki yamepatikana .

Kuna maswali mengi kuhusu jinsi, kwa nini na wakati hii ilitokea.

Hayo ni maswali ambayo tutayakusanya sasa wakati serikali zikikutana na kujadili jinsi ya kufanya uchunguzi.

Ajali hiyo ilitokea umbali gani na mabaki ya meli Titanic?

Eneo la ajali hiyo mbaya linaaminika kuwa futi 1600 (487m) kutoka upinde wa ajali ya Titanic.

Iko katika eneo ambalo hakuna mabaki yoyote ya meli ya Titanic.

Maafisa walisema vipande vitano vikuu viligunduliwa katikati ya vifusi karibu na eneo la mkasa wa Titanic.

Miongoni mwao, sehemu ya 'pua' la nyambizi hiyo sehemu ya nje ya 'chemba ya presha' ya chombo na mabaki mengine.

View Comments