In Summary

• Jonas Lutema, Mwanafamialia ambaye alishuhudiwa mazishi ya mwanamke huyo alisimulia kilichojiri.

• “Miaka 5 baadae, alionekana akiwa hai katika eneo la kuchotea maji akiwa na nguo alizozikwa nazo."

Marehemu arejea akiwa hai
Image: Screengrab

Maelfu ya watu walifurika katika wilaya la Mlele mkoa wa Katavi nchini Tanzania baada ya taarifa kuenea kwamba mwanamke aliyefariki mwaka 2018 na kuzikwa alionekana akiwa hai katika eneo la kuchotea maji, akiwa katika mavazi yale aliyozikwa nayo.

Unaweza usiamini lakini hili ni tukio ambalo lilishuhudiwa moja kwa moja na Ayo TV na waliripoti kwamba mwanamke huyo Mwashi Lutema mwenye umri wa miaka 33 alifariki dunia Aprili 2018 na kuzikwa.

“Miaka 5 baadae, alionekana akiwa hai katika eneo la kuchotea maji akiwa na nguo alizozikwa nazo. Hii imetokea Mkoani Katavi,” Ayo TV waliripoti.

Jonas Lutema, Mwanafamialia ambaye alishuhudiwa mazishi ya mwanamke huyo alisimulia kilichojiri.

“Huyu ndugu yetu mnamo 2018 alipatwa na homa ya kuugua mwili wote mara kifua, miguu na hatimaye ikaonekana kwamba ni mapepo. Tukaamua kumpeleka kwenye huduma ya triba asili na baadae hali ikawa mbaya mauti ikatokea. Tulimaliza kila itu jinsi ilivyo misiba ndugu tukawa tumesahau.”

“Kwa muda wa miaka 5, hatimaye mwezi huu tarehe 14 akawa ametokea sehemu akamkuta mdogo wake kisimani anachota maji, mdogo wake akamfananisha kweli huyu ni Fulani ikabidi waanze kusambaza simu hatimaye akachukuliwa akapelekwa ofisini na sisi ndugu tukapata taarifa na tukaenda tukakuta ni yeye na kila mtu akija anasema ni yeye,” mwanafamilia huyo alisema.

Baada ya hapo, gari la polisi liliwachukua na kumshusha kwa kaka yake ambapo watu wamekuwa wakifurika kama kituo cha utalii kushuhudia tukio hilo linalochukuliwa kama lisilo la kawaida.

Mwanafamilia huyo alisema kwamba kilichowapelekea kucmhukua kwa matibabu ya asili ni baada ya kugundua kwamba alikuwa na mapepo na wao wakaona mapepo na hospitali ni vitu viwii tofauti.

View Comments