In Summary

•Hatua hiyo inajiri miaka miwili baada ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kuunga mkono pingamizi la sheria iliyopo katika jimbo la kaskazini la Coahuila.

Image: BBC

Mahakama ya Juu Zaidi nchini Mexico imehalalisha uavyaji mimba kote nchini humo.

Hatua hiyo inajiri miaka miwili baada ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kuunga mkono pingamizi la sheria iliyopo katika jimbo la kaskazini la Coahuila.

Ilikuwa imetoa uamuzi kuwa adhabu za uhalifu kwa uavyaji mimba zilikuwa kinyume na katiba.

Majimbo ya Mexico na serikali kuu tangu wakati huo zimekuwa na mwendo wa kinyonga kufuta kanuni za adhabu.

Uamuzi huo mpya unahalalisha utoaji mimba katika majimbo yote 32.

Mahakama ya Juu Zaidi ilisema kukataliwa kwa uwezekano wa kutoa mimba kulikiuka haki za binadamu za wanawake.

"Katika kesi za ubakaji, hakuna msichana anayeweza kulazimishwa kuwa mama - sio na serikali wala na wazazi wake au walezi wake," mkuu wa mahakama hiyo, Arturo Zaldívar alisema.

"Hapa, ukiukwaji wa haki zake ni mbaya zaidi, sio tu kwa sababu ya hali yake kama mwathirika, lakini pia kwa sababu ya umri wake, ambayo inafanya kuwa muhimu kuchambua suala hilo kwa mtazamo wa masilahi bora ya watoto."

Hukumu hiyo inafungua mlango kwa mfumo wa afya wa serikali kutoa huduma za uavyaji mimba habari ambayo imepokelewa vizuri na vikundi vya kutetea haki za wanawake.

Mexico City ilikuwa jimbo la kwanza nchini humo kuhalalisha uavyaji mimba mwaka wa 2007 na mingine zaidi ikafuata mkondo huo.

View Comments