In Summary

• Muunganisho uliosimbwa kwa njia fiche husaidia kuhakikisha kuwa data nyeti inasambazwa kwa usalama.

Tanzania yamtaka kila mtumizi wa simu kutumia VPN
Image: BBC NEWS

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imetoa makataa ya hadi Oktoba 30 kwa watumiaji wote wa simu za rununu kujisajili kwenye huduma ya mtandao binafsi, VPN la sivyo watakwenda jela kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.

Mtandao pepe wa kibinafsi, au VPN, ni muunganisho uliosimbwa kwa njia fiche kupitia Mtandao kutoka kwa kifaa hadi kwa mtandao. Muunganisho uliosimbwa kwa njia fiche husaidia kuhakikisha kuwa data nyeti inasambazwa kwa usalama.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo mamlaka hiyo walipakia kupitia ukurasa wao rasmi wa X, awali ukijulikana kama Twitter, walitoa rai kwa watumizi wote wa simu kuhakikisha wamejisajili kwenye huduma hiyo ili kuweka salama data zao nyeti katika ulimwengu huu wa kidijitali ambapo data kudukuliwa ni rahisi sana.

“TCRA inautaarifu umma kwa ujumla, watu binafsi na makampuni ambayo kwa asili ya majukumu na kazi zao, matumizi ya mtandao binafsi, VPN hayazuiliki, kutoa taarifa kwa TCRA juu ya VPN wanazotumia na taarifa zote muhimu ikiwemo anuwani ya itifaki ya mtandao (IP address) kabla au mnano Oktoba 30,” sehemu ya waraka huo ilisoma.

Mamlaka hiyo ilisema kwamba itaendelea kuchukua hatua za kiudhibiti dhidi ya mitandao ya kibinafsi VPN yasiyo halali ikiwemo upatikanaji wa VPN ambazo hazijatolewa taarifa au kusajiliwa.

Mamlaka hiyo iliendelea kuwakumbusha watu kwamba kutojisajili kwenye huduma hiyo kutawafanya watu kuendelea kutoa au kusambaza teknolojia au program ambazo hazijachungwa na ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni kifungu kisichopungua miezi 12 jela au kutozwa faini ya shilingi milioni 5 za Kitanzania.

View Comments