logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu Pasta aliyeamuru wanamgambo kubaka watoto kama njia ya kujikinga dhiti ya risasi

Uchungizi wa 2013 ulionyesha watoto 40 walikuwa wamebakwa katika wilaya la Kavumu pekee.

image
na Davis Ojiambo

Habari30 March 2024 - 10:34

Muhtasari


  • • ‘Jeshi’ hilo ambalo lilikuwa linajihami vikali kwa silaha liliundwa na Batumike pamoja na mbunge wa Kivu Kusini kipindi hicho.
  • • Mwaka 2017, Batumike na wenzake 11 akiwemo mbunge walifikishwa mahakamani na Desemba mwaka huo walihukumiwa na mahakama ya kijesh
mkenya akamatwa kwa kumiliki dawa za kulevya

Mapema mwaka 2016, kisa cha kusikitisha kiliripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kikihusisha kundi moja la Kanisa kwa jina ‘Jeshi la Mungu’.

Katika ripoti hiyo ambayo imeibuliwa upya na gazeti la Daily Nation, kundi hili la kanisa ambalo lilitajwa kuwa la wanamgambo lilitumbuliwa kwa kushiriki msururu wa visa dhidi ya ubinadamu kwa wanawake na watoto.

Likiwa na ngome yake pembezoni mwa ziwa Kivu, Jeshi la Yesu walikuwa wakiongozwa na mchungaji mmoja kwa jina Frederic Batumike ambaye baadae 2017 yeye pamoja na wanachama wengine 11 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa shtaka la dhuluma dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa mujibu wa ripoti, pasta huyo alikuwa akitoa mafunzo yenye itikadi kali kwa ‘Jeshi la Yesu’ kuwakamata na kuwabaka watoto kama njia moja ya kujihakikishia kinga dhidi ya risasi, kwa kimombo ‘bullet-proof’.

‘Jeshi’ hilo ambalo lilikuwa linajihami vikali kwa silaha liliundwa na Batumike pamoja na mbunge wa Kivu Kusini kipindi hicho.

Inaarifiwa kwamba ‘uchafu’ wao ulianza mwaka 2012 wakati Batumike, pasta mwenye kimo cha mbilikimo, alipowapeleka wanachama wake kwa mganga wa kinyeji ambaye aliwaambia kwamba ili kujikinga dhidi ya risasi na silaha zingine, ingewabidi kuwabaka watoto, Nation waliripoti.

“Mganga huyo kisa akawahadaa kuchanganya damu ya ubikira na mitishamba, akisema kwamba kwa kufanya hivyo, wangekuwa wapiganaji wasioshindwa vitani. Pasta Batumike akawaamuru wanachama wake kuanza kuvamia majumba wakitelekeza oparesheni yao ya ubakaji dhiti ya watoto mabikira,” sehemu ya ripoti ya jarida hilo ilisoma.

Wanamgambo wa ‘jeshi la Yesu’ waliendeleza uvamizi wao na kuwatorosha hadi watoto 20 katika wilaya la Kavumu, huku baadae miili yao ikipatikana imetupwa baada ya kubakwa.

Uchunguzi wa mwaka 2013 uliofanywa na Physicians for Human Rights katika eneo la Kivu ulibaini kwamba Zaidi ya watoto 40 walibakwa na kuuawa na Jeshi la Yesu katika wilaya la Kavumu pekee.

Mwaka 2017, Batumike na wenzake 11 akiwemo mbunge walifikishwa mahakamani na Desemba mwaka huo walihukumiwa na mahakama ya kijeshi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved