In Summary

•Trump ametoa moja ya mahojiano yake ya kwanza tangu jaribio la kumuua Jumamosi usiku, akisema ameandika upya kabisa hotuba yake.

•Donald Trump amesema "alitakiwa kuwa amefariki", akitaja jaribio la mauaji kuwa "kitu kibaya" kukipitia.

Image: BBC

Rais wa zamani Donald Trump ametoa moja ya mahojiano yake ya kwanza tangu jaribio la kumuua Jumamosi usiku, akisema ameandika upya kabisa hotuba yake ya mkutano ili kuzingatia ujumbe wa "umoja" badala ya kumkosoa Joe Biden.

"Hotuba ambayo ningetoa Alhamisi itakuwa ya kufurahisha," aliiambia Washington Examiner.

"Kama haya hayangetokea, hii ingekuwa mojawapo ya hotuba za kushangaza," alisema pia, akiongeza kuwa ingelenga zaidi sera za Rais Biden.

"Kusema kweli, itakuwa hotuba tofauti kabisa sasa. Ni nafasi ya kuleta nchi pamoja. Nilipewa nafasi hiyo.”

Trump pia alisema kwamba "ukweli" wa kile kilichotokea Jumamosi " ndio unaanza tu," na akaelezea wakati alipotazama umati wa watu baada ya kugundua kuwa alikuwa amepigwa risasi.

“Nguvu iliotoka kwa watu waliokuwepo wakati huo, walisimama tu; ni vigumu kuelezea jinsi nilivyohisi, lakini nilijua ulimwengu ulikuwa unatazama. Nilijua kuwa historia ingehukumu hili, na nilijua lazima niwafahamishe tuko sawa,” alimwambia Mkaguzi.

Donald Trump amesema "alitakiwa kuwa amefariki", akitaja jaribio la mauaji kuwa "kitu kibaya" kukipitia.

"Sitakiwi kuwa hapa, ninapaswa kuwa nimekufa," Trump alisema, akizungumza na New York Post alipokuwa akielekea Milwaukee kwa Kongamano la Kitaifa la Republican.

Trump alivaa bandeji nyeupe iliyofunika sikio lake la kulia lakini wasaidizi wake hawakuruhusu picha zozote kupigwa, lilisema Post.

"Daktari katika hospitali alisema hajawahi kuona kitu kama hiki, alikitaja kuwa muujiza," Trump aliongeza.

View Comments