In Summary

•Kwa miaka mingi, India imekuwa mshirika wake mkubwa na hii imefanya kazi vizuri kwa nchi zote mbili.

•Wakati wa utawala wake, Hasina alikabiliana na makundi ya wapiganaji wanaopinga India huko Bangladesh.

Image: BBC

Kulingana na ripoti, "mahali salama" Sheikh Hasina anakoelekea ni jirani yake mkubwa - India.

Kwa miaka mingi, India imekuwa mshirika wake mkubwa na hii imefanya kazi vizuri kwa nchi zote mbili.

Bangladesh inashiriki mipaka na idadi ya majimbo ya kaskazini-mashariki ya India - ambayo mengi yamepambana na wanamgambo kwa miongo kadhaa, na serikali ya kirafiki huko Dhaka imekuwa ikisaidia kwa hilo.

Wakati wa utawala wake, Hasina alikabiliana na makundi ya wapiganaji wanaopinga India huko Bangladesh, hatua ambayo ilimleta karibu na utawala mjini Delhi.

Pia ametoa haki za usafiri kwenda India kuhakikisha bidhaa kutoka bara zinafika katika majimbo hayo.

Hasina, ambaye alianzisha uhusiano wa karibu na India tangu alipochaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1996, amekuwa akihalalisha uhusiano wa karibu wa Dhaka na Delhi.

Wakati wa ziara yake nchini India mnamo 2022, aliwakumbusha watu wa Bangladesh jinsi India, serikali yake, watu na vikosi vya jeshi viliisaidia nchi wakati wa vita vya uhuru mnamo 1971.

Lakini ukaribu wake na Delhi - na uungwaji mkono wake na India - umekosolewa na vyama vya upinzani na wanaharakati ambao wanasema India inapaswa kuwaunga mkono watu wa Bangladesh na sio chama fulani.

View Comments