logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa afungwa jela kwa kumpiga ngumi Waziri Mkuu wa Denmark

Mahakama ya ilimhukumu kifungo cha miezi minne jela, kufukuzwa nchini na kupigwa marufuku kuingia Denmark kwa miaka mitano.

image
na Samuel Maina

Habari08 August 2024 - 04:06

Muhtasari


  • •Mahakama ya Copenhagen ilimhukumu kifungo cha miezi minne jela, kufukuzwa nchini na kupigwa marufuku kuingia Denmark kwa miaka mitano.

Mwanaume mmoja raia wa Poland amepatikana na hatia ya kumpiga ngumi Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen.

Mahakama ya Copenhagen ilimhukumu kifungo cha miezi minne jela, kufukuzwa nchini na kupigwa marufuku kuingia Denmark kwa miaka mitano.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye hakutajwa jina, aliimbia mahakama siku ya Jumanne kwamba alikuwa amelewa sana kukumbuka kilichotokea.

Bi Frederiksen alipata majeraha madogo alipopigwa ngumi begani wakati wa shambulio hilo katika uwanja mmoja mjini humo mwezi Juni.

Pamoja na shtaka la unyanyasaji dhidi ya mtumishi wa umma, mtu huyo pia alipatikana na hatia kwa makosa kadhaa ya ulaghai na utovu wa nidhamu unaohusiana na matukio mengine.

Baada ya kutumikia kifungo chake jela atafukuzwa nchini. Pia atalazimika kulipa gharama za kesi.

Bi Frederiksen hakutoa ushahidi katika kesi hiyo. Mshtakiwa alikana shtaka la kushambulia lakini alikiri mashtaka mengine.

Alisema alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi ya kutoweza kukumbuka kilichotokea na kwamba alikuwa na "siku mbaya" alipokutana ana kwa ana na Bi Frederiksen.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved