logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mgonjwa wa kwanza wa Mpox apatikana Sweden

Takribani watu 450 walikufa wakati wa mlipuko wa awali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

image
na Davis Ojiambo

Habari16 August 2024 - 04:21

Muhtasari


  • • Shirika la WHO limetangaza mlipuko wa ugonjwa wa mpox katika baadhi ya maeneo ya Afrika kuwa dharura ya afya ya umma.
Dalili za mpox ni pamoja na upele unaoanzia usoni na kusambaa mwilini.

Wakala wa afya ya umma nchini Sweden imerekodi kile inachosema kuwa ni kisa cha kwanza cha aina mpya ya ugonjwa wa mpox nje ya bara la Afrika.

Mtu huyo aliambukizwa alipokuwa akikaa katika eneo la Afrika ambako kwa sasa kuna mlipuko mkubwa wa mpox Clade I, shirika hilo lilisema.

Habari hizo zinakuja saa chache baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza kwamba mlipuko wa ugonjwa wa mpox katika baadhi ya maeneo ya Afrika sasa ni dharura ya afya ya umma ambayo inatia wasiwasi kimataifa.

Takribani watu 450 walikufa wakati wa mlipuko wa awali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved