logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Benki kuu ya Libya yasitisha shughuli baada ya mkurugenzi kutekwa nyara

Bw Msallem alichukuliwa kutoka nyumbani kwake na "watu wasiojulikana" Jumapili asubuhi na wafanyakazi wengine pia wametishiwa kuteka nyara.

image
na Samuel Maina

Habari19 August 2024 - 11:52

Muhtasari


  • •Bw Msallem alichukuliwa kutoka nyumbani kwake na "watu wasiojulikana" Jumapili asubuhi na wafanyakazi wengine pia wametishiwa kuteka nyara.

Benki kuu ya Libya imetangaza kusimamisha shughuli zake zote baada mfanyakazi wake wa ngazi ya juu kutekwa nyara katika mji mkuu Tripoli.

Benki hiyo ililaani kutekwa nyara kwa mkurugenzi wake wa teknolojia ya habari Musab Msallem katika taarifa yake siku ya Jumapili.

Imesema Bw Msallem alichukuliwa kutoka nyumbani kwake na "watu wasiojulikana" Jumapili asubuhi na kwamba wafanyakazi wengine piA wametishiwa kuteka nyara.

Benki kuu inasema shughuli hazitaendelea hadi Bw Msallem aachiliwe.

Benki kuu, ambayo ni huru lakini inayomilikiwa na taifa la Libya, ndiyo hifadhi pekee inayotambulika kimataifa kwa mapato ya mafuta ya Libya ambayo ni muhimu ya kiuchumi kwa nchi iliyosambaratishwa kwa miaka inayoongozwa na serikali mbili hasimu za Tripoli na Benghazi.

Hii inakuja wiki moja baada ya benki kuu kuzingirwa na watu wenye silaha, kulingana na shirika la habari la AFP.

Tangu kuondolewa madarakani na kuuawa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi mwaka 2011, nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved