logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Iran ilidukua kampeni ya Trump, ujasusi wa Marekani wathibitisha

Maafisa wa Kampeni ya Trump waliinyooshea kidole Iran tarehe 10 Agosti kwa kudukua jumbe zake za ndani.

image
na Samuel Maina

Habari20 August 2024 - 04:47

Muhtasari


  • •Maafisa wa Kampeni ya Trump waliinyooshea kidole Iran tarehe 10 Agosti kwa kudukua jumbe zake za ndani.

Iran ilihusika na udukuzi wa hivi majuzi wa kampeni za urais za Donald Trump, maafisa wa kijasusi wa Marekani wamethibitisha.

FBI na mashirika mengine ya shirikisho yalisema katika taarifa ya pamoja kwamba Iran imechagua kuingilia uchaguzi wa Marekani "ili kuchochea mifarakano na kudhoofisha imani kwa taasisi zetu za kidemokrasia".

Maafisa wa Kampeni ya Trump waliinyooshea kidole Iran tarehe 10 Agosti kwa kudukua jumbe zake za ndani. Maafisa wa Iran walikanusha.

Vyanzo vinavyofahamu uchunguzi huo viliiambia kampuni ya habari mshirika wa BBC wa Marekani, CBS News, kwamba wanashuku kuwa wavamizi wa kitandao wa Iran pia waliilenga kampeni ya mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris.

"[Jumuiya ya kijasusi] ina imani kwamba Wairani kupitia uhandisi wa kijamii na juhudi zingine walitafuta ufikiaji wa taarifa za watu binafsi wenye uwezo wa moja kwa moja wa kampeni za Urais za pande zote mbili za kisiasa," maafisa wa ujasusi wa Marekani walisema katika taarifa hiyo.

"Shughuli kama hizo, ikiwa ni pamoja na wizi na ufichuzi, zinalengo la kuathiri mchakato wa uchaguzi wa Marekani."

Bado haijulikani ni habari gani, ikiwa zipo, ziliibiwa wakati wa udukuzi. Trump alisema wadukuzi hao waliweza tu kupata taarifa zinazopatikana kwa umma.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved