logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Oprah awasihi wapiga kura 'kuchagua ukweli' katika kongamano la Democrats

Tuchague ukweli, tuchague heshima, tuchague furaha," Winfrey aliuambia umati.

image
na Davis Ojiambo

Habari23 August 2024 - 07:24

Muhtasari


  • "Tuchague ukweli, tuchague heshima, tuchague furaha," Winfrey aliuambia umati uliokuwa ukishangilia siku ya Jumatano.

Nguli wa televisheni Oprah Winfrey amejitokeza bila kutarajiwa katika Kongamano la Kitaifa la chama cha Democrats katika mji alikozaliwa wa Chicago, ambapo aliwataka wafuasi wa chama hicho na wapiga kura wasioegemea upande wowote "kuchagua busara badala ya upuuzi".

"Tuchague ukweli, tuchague heshima, tuchague furaha," Winfrey aliuambia umati uliokuwa ukishangilia siku ya Jumatano. "Kwa sababu hiyo ndiyo Marekani bora zaidi."

Winfrey, ambaye ameepuka kujiingiza kwenye kisiasa katika miaka ya hivi majuzi, alionyesha kujionea fahari Makamu wa Rais Kamala Harris na mgombea mwenza wake, gavana wa Minnesota Tim Walz katika usiku wa tatu wa kongamano la siku nne.

Kuwaunga mkono wawili hao kumesaidia kuipa nguvu zaidi chama cha Democtrats - ambacho wiki hii kimeshuhudia kujitokeza kwa watu wengi maarufu kama vile rapper Lil Jon.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved