In Summary

•Kati ya watoto hao wanne, wawili walikosa hewa hadi kufa kwenye friji huku wengine wawili wakifia hospitalini.

Image: BBC

Polisi nchini Namibia wanachunguza kifo cha watoto wanne waliokuwa wakicheza kwenye jokofu tupu katika Mkoa wa Zambezi kaskazini-mashariki.

Watoto hao wenye umri wa kati ya miaka mitatu na sita, walipatikana ndani ya friji isiyotumika katika eneo lenye watu wengi katika mji wa Katima Mulilo siku ya Jumatatu alasiri.

Polisi wanaamini kuwa watoto hao walinaswa kwa bahati mbaya walipokuwa wakicheza na kuzidiwa ndani lakini uchunguzi unaendelea.

Kati ya watoto hao wanne, wawili walikosa hewa hadi kufa kwenye friji huku wengine wawili wakifia hospitalini wakipokea matibabu, shirika la utangazaji la umma liliripoti.

"Nilipoingia, niliwaona wahudumu wa afya wakihudumia binti yangu na msichana mwingine. Waliwakimbiza hospitalini, huku wengine wawili wakiwa wamepakiwa kwenye magari ya polisi ya kuhifadhia maiti,” Aranges Shoro, baba wa watoto hao, aliambia gazeti la kibinafsi la The Namibian.

Wawili hao ambao walikimbizwa katika hospitali ya karibu ya Jimbo la Katima Mulilo walitangazwa kufariki walipofika, tovuti ya habari ya shirika la utangazaji la umma NBC iliripoti .

Haijabainika kwa nini friji hiyo isiyofanya kazi iliachwa nje ya nyumba ya mojawapo ya familia zilizoathirika

View Comments