In Summary

• Viongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu na Freeman Mbowe wamekamatwa asubuhi ya Jumatatu nyumbani kwao.

• Chama cha CHADEMA kilitangaza kuwepo kwa maandamano maombolezo kufanyika Jumatatu 23.

Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA
Image: BBCSwahii

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA cha Tanzania  kimeripoti kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu amekamatwa na jeshi la polisi.

CHADEMA imeripoti hayo mapema asubuhi ya Jumatatu ikiarifu kuwa jeshi la polisi halikutoa taarifa ya ni kituo kipi cha polisi kiongozi huyo wa chama cha upinzani nchini Tanzania anazuiliwa.

Kupitia ukurasa wa X, CHADEMA imeandika kuwa Lissu alikamatwa nyumbani kwake eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam na kuchukuliwa na msafara wa magari kumi na moja.

Vile vile, CHADEMA imearifu kuwa mke wa mwenyekiti wa Chama cha Taifa  nchini Tanzania Freeman Mbowe pia amezuiliwa.

Dr. Lilian Mtei,mkewe Freeman ,kulingana na CHADEMA, alizuiliwa na jeshi la polisi la Tanzania akiwa anatoka nyumbani kwake Mikocheni, Dar es Salaam.

Vyombo vya habari nchini Tanzania vimearifu kuwa Freeman Mbowe alikamatwa na jeshi la polisi katika eneola Magomeni Mapipa baada ya kuonekana akiongea na waandishi wa habari.

Freeman alikuwa ameandamana na mwanawe Nicole Mbowe ambaye pia alikamatwa wakati alikuwa anaondoka kwa kutumia boda boda.

CHADEMA mnamo tarehe 13 Septemba, ilitangaza maandamano ya Maombolezo jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kufanyika Jumatano tarehe 23 Septemba maandamano ambayo jeshi la polisi la Tanzania lilipiga marufuku maandamano hayo kufanyika.

View Comments