In Summary

•Fahim alikuwa akishiriki mchezo wa kujificha na kutafuta pamoja na kundi la marafiki zake katika eneo la Chittagong, nchini Bangladesh.

•Fahim ambaye alionekana kuchanganyikiwa  sana hakuzungumza wala kuelewa lugha ya wafanyakazi hao.

Kijana Ajificha Kwenye Kontena Wakati wa Mchezo wa Ficha na Utafute, Ajipata Nchi Nyingine
Image: HISANI

Mvulana mmoja wa miaka 15 kutoka Bangladesh amewashangaza wengi kwa kusafirishwa hadi nchi nyingine bila kujua baada ya kufungiwa ndani ya kontena ya mizigo.

Fahim, kama alivyotambuliswa na vyombo vya habari vya Malysia alikuwa akishiriki mchezo wa kujificha na kutafuta pamoja na kundi la marafiki zake katika eneo la Chittagong, nchini Bangladesh mnamo Januari 11 alipopata wazo la kujificha ndani ya kontena la mizigo lililokuwa wazi, akihisi ni maficho mazuri.

Imeripotiwa kuwa alijifungia ndani ya kontena hiyo kwa bahati mbaya kisha akapatwa na usingizi kabla ya wafanyakazi wa bandari kupakia kontena hilo kwenye meli iliyokuwa ikielekea Malysia, takriban kilomita 3033.576 kutoka nyumbani.

Meli hiyo ilianza safari yake  kutoka bandari ya Chittagong mnamo Januari 11 na kufika Port Klang nchini Malaysia mnamo Januari 17 wakati mvulana huyo alipogunduliwa. Wafanyakazi wa bandari walishangaa sana kumuona kijana aliyechanganyikiwa na aliyedhoofika akitoka kwenye moja ya kontena.

Fahim ambaye alionekana kuchanganyikiwa  sana hakuzungumza wala kuelewa lugha ya wafanyakazi hao, kwa hiyo ilikuwa vigumu sana kuwasiliana nao.

Maafisa ambao tayari walikuwa wameanza kushuku kwamba alikuwa mhasiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu mara moja walipiga simu kwa polisi ambapo baadaye ukweli ulibainika kuhusu yaliyompata Fahim.

Baadaye alichukuliwa nankupelekwa katika hospitali kwa gari la wagonjwa kabla ya mipango ya kumrejesha Bangladesh kufanywa. 

Fahim alifungiwa ndani ya kontena hiyo kwa siku sita huku akipiga kelele kuomba msaada kutoka ndani lakini hakuna yeyote aliyemsikia. Jinsi alivyoishi kwa wiki moja bila tonge la chakula au maji bado ni kitendawili ambacho hakijaweza kuteguliwa

View Comments