In Summary

• Mwanaume huyo walizozana na mkewe baada na mkewe huyo kumuomba pesa za kulipa kodi ya nyumba, kiasi cha shilingi elfu mbili.

Kisu cvha mauaji
Image: Maktaba

Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kwamba ongezeko la visa vya mauaji ya kinyumbani ni kutokana na ugumu wa maisha, unyongovu na msongo wa mawazo miongoni mwa Wakenya wengi ambao wanasukumwa na moja kati ya vyanzo hivyo hadi kufikia uamuzi wa kutekeleza mauaji ya watu wa karibu naye au hata kujiua wenyewe.

Usiku wa kuamkia Jumanne, mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Kirinyaga alifanya kufuru ya mwaka baada ya kumuua bintiye mdogo kwa kile kilisemekana kwamba ni ugomvi wa nyumbani na mkewe, mamake marehemu.

Mwanaume huyo walizozana na mkewe baada na mkewe huyo kumuomba pesa za kulipa kodi ya nyumba, kiasi cha shilingi elfu mbili.

Hapo ndipo alicharuka juu na kughasiwa na mori ambapo alichukua kisu na kumdunga mara kadha bintiye wa mwaka mmoja unusu mpaka kufa baada yake kujaribu pia kujitoa uhai lakini akazuiliwa na watu waliowahi kufika katika eneo la tukio.

Alikimbizwa hospitalini na mwili wa mtoto huyo ukapelekwa katika cvhumba cha kuhifadhi maiti huku akisubiriwa kupona kabla ya kushtakiwa kwa kosa la mauaji na kujaribu kujiua pia.

View Comments