In Summary
  • Washukiwa 4 wafikishwa mahakamani kwa kujaza tena gesi za LPG kinyume cha sheria
Washukiwa 4 wafikishwa mahakamani kwa kujaza tena gesi za LPG kinyume cha sheria
Image: DCI

Washukiwa wanne walifikishwa katika mahakama ya Mavoko Law siku ya Jumatano kwa kujaza tena mitungi ya gesi kinyume cha sheria katika kiwanda cha kujaza eneo la Mlolongo, kaunti ya Machakos.

Mkurugenzi wa kampuni ya Green Gas Abdikalik Mohamed pamoja na wenzake Bidan Ndungu, Abdistar Maalim na Adankheir Mohammed, walishtakiwa kwa kuendesha ghala kubwa la kuhifadhia gesi ya Liquefied Petroleum (LPG) bila leseni halali na kujaza bidhaa mbalimbali za gesi bila kibali. 

Wanne hao waliachiliwa kwa dhamana ya Ksh.100,00 pesa taslimu baada ya kukanusha mashataka, kulingana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI).

Wakati huo huo, lori lililokuwa likitumika kusafirisha mitungi hiyo limezuiliwa pamoja na jumla ya mitungi 96 mali ya makampuni mengine.

"Bidan Ndungu, Abdistar Maalim na Adankheir Mohammed walikamatwa na lori kupatikana likisafirisha mitungi kuzuiwa. Washukiwa hao wameachiliwa kwa dhamana ya Sh100,000 pesa taslimu.

Baada ya jumla ya mitungi 96 ya makampuni mengine kunaswa kutoka kwa majengo yake. Katika operesheni hiyo iliyoendeshwa na maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha Makosa Makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita, washukiwa wengine watatu waliopatikana wakijaza mitungi kwenye mtambo huo pia waliwekwa korokoroni," DCI Alisema.

 

 

View Comments