In Summary

•Muzami alinaswa akimgonga mhasiriwa kwa bunduki kwenye paji la uso huku Humphrey akinaswa akiwa ameshikilia kisu kwenye koo la mhasiriwa.

•Miongoni mwa vifaa vya kielektroniki vilivyoibiwa ni pamoja na Macbook, iPhone, kibodi, mouse, miwani pamoja na vitu vingine.

Timothy Musami na Humphrey Minyata mbele ya hakimu wa Milimani Zainab Abdul Alhamisi Juni 9, 2022.
Image: DOUGLAS OKIDY

Habari na Caroline Chepchirchir

Wanaume wawili waliokuwa na silaha ambao walinaswa kwenye  CCTV wakimwibia mwanaume mwingine katika eneo la Kilimani wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Timothy Jahan Muzami, 28, na Humphrey Minyata, 25, walirekodiwa na CCTV wakiiba vifaa vya kielektroniki vya thamani ya Sh396,733 kutoka kwa mwanaume aliyekuwa  akitembea kando ya Barabara ya Lenana mnamo Juni 25, 2020.

Muzami alinaswa akimgonga mhasiriwa kwa bunduki kwenye paji la uso huku Humphrey akinaswa akiwa ameshikilia kisu kwenye koo la mhasiriwa.

Miongoni mwa vifaa vya kielektroniki vilivyoibiwa ni pamoja na Macbook, iPhone, kibodi, mouse, miwani pamoja na vitu vingine.

Vifaa hivyo vilikuwa kwenye begi ambalo mlalamishi alionekana akisalimisha kwa washukiwa hao.

Hakimu mkuu Zainab Abdul alisema silaha ya washukiwa haikupatikana tena na inaendelea kutumika mitaani na kuhatarisha maisha ya watu wengi.

Wakati wa mahojiano, Hakimu alisema familia ya washtakiwa iliomba mahakama iwape adhabu ya kutokuwa rumande.

Hata hivyo, mahakama ilisema kutokana na kosa lao pamoja na ushahidi uliotolewa, kesi hiyo isitolewe adhabu ya kutokuwa rumande.

"Kufuatia matukio ya hivi majuzi, kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu wanaoibiwa kwa kutumia bunduki huku bodaboda zikiwasaidia kutoroka," hakimu alisema.

"Kwa hiyo, mahakama ina mamlaka ya kutoa adhabu ambayo itakuwa onyo kwa yeyote atakayetenda kosa kama hilo."

View Comments