In Summary

•Stephen Wanyonyi Munyolo alishtakiwa siku ya Jumatatu mbele ya hakimu mkuu wa Kibera Ann Mwangi ambapo alikanusha mashtaka.

•Alishtakiwa kwa kosa la pili la kufanya kitendo cha aibu na mtoto huyo kinyume na sheria.

Mshukiwa Stephen Wanyonyi Munyolo katika mahakama ya Kibera mnamo Oktoba 17, 2022.
Image: CLAUSE MASIKA

Askofu maarufu anayeongoza kanisa moja lililo ndani ya mtaa wa Kibera alikabiliwa na mashtaka ya kumnajisi msichana wa miaka 10 katika mahakama ya Kibera.

Stephen Wanyonyi Munyolo alishtakiwa siku ya Jumatatu mbele ya hakimu mkuu wa Kibera Ann Mwangi ambapo alikanusha mashtaka.

Hati ya mashtaka iliyosomwa kortini inasema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa tarehe tofauti kati ya Septemba 8 na Oktoba 2022 katika eneo la Silanga huko Kibera, kaunti ndogo ya Lang'ata.

Alishtakiwa kwa kosa la pili la kufanya kitendo cha aibu na mtoto huyo kinyume na sheria.

Mtumishi huyo wa Mungu ameoa wake wawili pamoja na ambaye ana watoto 14.

Mahakama, hata hivyo, ilisikia kwamba amekuwa akimnajisi msichana huyo mara kadhaa.

Upande wa mashtaka, hata hivyo, haukupinga kuachiliwa kwake kwa dhamana lakini ulitaka masharti magumu ya dhamana.

Hakimu alimwachilia kwa bondi ya Sh300,000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho bila dhamana ya pesa taslimu.

Kisha mshtakiwa aliuliza kujua kama anaweza kutumia hati yake ya umiliki kujidhamini mwenyewe jambo ambalo mahakama ilikubali.

Hakimu aliagiza kesi hiyo itajwe Oktoba 28 kwa maelekezo zaidi.

View Comments