In Summary

•Raphael Tuju aliwatembelea makamishna wanne wa IEBC katika nyumba ambayo walikuwa wamepangiwa kwenye jumba la Yaya, mahakama iliambiwa.

•Mahakama  pia iliarifiwa kuwa Okwe ndiye aliyeandikisha kikao na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena.

Makamishna wa IEBC Justus Nyangaya, makamu mwenyekiti Juliana Cherera, Irene Masit na Francis Wanderi wakati wa mkutano uliopita na wanahabari katika hoteli ya Serena.
Image: REUTERS

Mkurugenzi mtendaji wa Azimio-One Kenya Raphael Tuju aliwatembelea makamishna wanne wa IEBC katika nyumba ambayo walikuwa wamepangiwa kwenye jumba la Yaya, mahakama iliambiwa.

Inadaiwa walikaa katika vyumba hivyo kwa siku nne kuanzia Agosti 15 hadi 19, ambapo walitembelewa na Tuju na pamoja na katibu mkuu wa Kanu aliyetimuliwa Nick Salat.

Alhamisi, mfanyakazi katika Yaya Centre aliambia mahakama inayoongozwa na Jaji Aggrey Muchelule kwamba makamishna watatu wa zamani Juliana Cherera, Francis Wanderi na Justus Nyang'aya pamoja na Irene Masit walikaa pale kwa siku nne.

Makamishna wawili ambao sasa wamejiuzulu pamoja na aliyekuwa makamu mwenyekiti Cherera isipokuwa Masit wanachunguzwa kuhusu mienendo yao baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati mwezi Agosti.

Meneja wa malazi Simon Ngila aliambia mahakama kuwa mmoja wa wateja wao waliorejea Edwin Okwe ndiye aliyepanga vyumba vitatu kwa niaba ya makamishna hao.

Video za CCTV kutoka kwenye vyumba ambazo zilivyochezwa kwenye kikao hicho zinadaiwa kumuonyesha Masit akitembea kwenye lifti ambayo ingempeleka chumbani, hata hivyo, video hiyo haikuwa wazi.

Ngila alisema wafanyakazi kadhaa waliokuwa wakifanya kazi siku hiyo walithibitisha kuwaona makamishna hao wakiingia kwenye kituo hicho na kwenda kwenye nyumba zao.

Aidha alisema kuwa Okwe aliingia mwendo wa saa mbili na dakiks 39 jioni siku ya taarifa kwa waandishi wa habari na kusema alikuwa akipanga vyumba vya VIP lakini hakutaja majina.

Ilidaiwa kuwa Tuju alifika kuwatembelea makamishna hao wakiwa wamekaa katika ghorofa hiyo.

"Tuju aliwatembelea makamishna wote wanne kulingana na rekodi," Ngila alidai.

Ngila pia alieleza kuwa Salat pia aliwatembelea makamishna hao wakati wa kukaa kwao.

Hata hivyo, Ngila alisema makamishna hao hawakuwahi kuweka rekodi zozote wakati wa wageni kuingia kama ulivyo utaratibu na walitiliwa saini na walinzi wao.

"Timu yetu ilitambua makamishna wanne wa IEBC kwa kuwa hatukuweza kupata rekodi zetu. Kwa sababu hazikuwekwa kwenye rekodi na walinzi walisema wangezipata siku iliyofuata," alisema.

Mahakama hiyo pia iliarifiwa kuwa Okwe huyohuyo ndiye aliyeandikisha kikao na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena.

Alidai kuwa mnamo Agosti 15 mwanamume huyo ambaye baadaye alitambuliwa kwa jina la Okwe aliingia katika hoteli hiyo katika eneo la mapokezi na kuuliza ni kiasi gani uwanja huo ungegharimu kikao na waandishi wa habari .

Chege alisema Okwe alienda mbele na kulipia uwanja kwa ajili ya kikao hicho kwa siku mbili.

Akihojiwa, wakili wa Masit Donald Kipkorir alimuuliza Ngila kwa nini waliwapa walalamishi picha hiyo ya video bila kibali cha mahakama.

Pia alibainisha kuwa jina la mbunge wa Kapseret Oscar Sudi pia lilikuwa kwenye rekodi lakini Ngila akafafanua kuwa Sudi alikuwepo siku chache baada ya makamishna hao kukagua kituo hicho.

Ngila alifafanua zaidi kwa mahakama hiyo kwamba tarehe za pekee katika kesi hiyo ni kati ya Agosti 15 na 19 lakini kukaa kwa Sudi hakuhusiani na makamishna hao hata kidogo.

Mkurugenzi Mtendaji wa IEBC Marjan Marjan pia alijitokeza kutoa ushahidi dhidi ya Masit ambaye alikuwepo kwenye vikao vya mahakama hiyo.

Marjan alisema alishangaa kuona makamishna wanne wakitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika hoteli ya Serena kupinga matokeo wakati walikuwa wamefanya kazi kwa karibu hadi mwisho.

"Kwa kweli nilishangaa kuona makamishna wanne wakipinga matokeo ya Serena,"

Marjan alidai kuwa kila kitu kilikuwa kizuri hadi alipojaza fomu 34 C ndipo makamishna hao wanne waliposema tofauti ya kura 233,000 kati ya wagombea urais wawili ilikuwa ndogo sana.

Aidha alidai kuwa wanne hao waliomba Chebukati kuruhusu marudio kutokana na kura ndogo lakini mwenyekiti akakataa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi mwaka ujao.

View Comments