In Summary
  • Lakini wakili wa upande wa mashtaka James Gachoka alikuwa amepinga kurejeshwa kwa simu hizo akisema ni sehemu ya uchunguzi
Mahakama
Image: MAHAKAMA

Maafisa wanne wa polisi waliokamatwa kwa madai ya kujaribu kuwaibia wafanyikazi wa ofisi ya kubadilisha fedha za kigeni jijini Nairobi wameachiliwa bila masharti.

Hii ni baada ya mahakama kuambiwa kuwa hakuna ushahidi wa kuwahusisha na makosa yanayodaiwa kuwa ya wizi.

Maafisa wanne; Daniel Wambui, Eliud Kipkurui, Stanley Gitonga na Nicholas Murira walikamatwa mnamo Januari 9, 2023.

Mahakama iliagiza kwamba simu za rununu zinazoshikiliwa na polisi zirudishwe kwao ndani ya siku 14.

Afisa huyo alisema simu hizo zilichukuliwa kwa uchunguzi wa kitaalamu baada ya kukamatwa.

Wakili wa utetezi Zachariah Mwambi alikuwa ametuma maombi ya kutaka simu hizo zirudishwe kwa washukiwa kwa sababu hawakuweza kuwasiliana na jamaa zao.

Lakini wakili wa upande wa mashtaka James Gachoka alikuwa amepinga kurejeshwa kwa simu hizo akisema ni sehemu ya uchunguzi.

 

 

 

View Comments