In Summary
  • Wakati huo huo, mabaki ya bintiye yalihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya Kitengela.
Image: KWA HISANI

Mahakama ya Kajiado imeamuru kuzuiliwa kwa mwanamke anayekabiliwa na shtaka la mauaji baada ya kudaiwa kumuua bintiye wa miaka miwili kwa kumkata vipande vipande kwa kisu na kisha kula sehemu za viungo vyake vya ndani.

Olivia Naserian anadaiwa kumuua bintiye Glory Njeri nyumbani kwao Kitengela eneo la Milimani Estate siku ya Jumapili, kisha kumlaza ndani kabla ya majirani kuwaarifu polisi, ambao walifika eneo la tukio na kumkamata.

Alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Jane Kamau Jumanne ambaye aliamuru Naserian abaki rumande ya polisi kwa siku 10 nyingine ili kuruhusu maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi wao.

Naserian anatarajiwa kuhudhuria kesi hiyo Mei 8.

Wakati huo huo, mabaki ya bintiye yalihamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya Kitengela.

 

 

 

 

View Comments