In Summary

•Ringtone alishtakiwa pamoja na Samson Onunga almaarufu Kazola, Victor B Maringa, Kevin Nyaoke, Brian Jumba Luseno na Geoffrey Mose.

Ringtone Apoko alifikishwa mahakamani Julai 25, 2023
Image: CLAUSE MASIKA

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Alex Apoko, almaarufu Ringtone ameshtakiwa mahakamani kwa tuhuma za kuwashambulia raia kadhaa wa Sudan na kuharibu viti vya thamani ya Sh50000.

Mwanamuziki huyo alishtakiwa pamoja na Samson Onunga almaarufu Kazola, Victor B Maringa, Kevin Nyaoke, Brian Jumba Luseno na Geoffrey Mose.

Watano hao walikanusha mashtaka na kupitia kwa wakili wao waliomba wapewe masharti ya dhamana.

Walishtakiwa kuwa mnamo Julai 21 katika ghorofa moja eneo la Bomas, kaunti ndogo ya Langata, jijini Nairobi waliwashambulia Kongkong Paulino, Gabriel Paulino, Stephen Gatwech, John Paulino na Chuang Emmanuel na kuwadhuru mwili.  Kiti kilichoharibika kilikuwa cha familia ya Kongkong.

Waliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh50,000 kila mmoja.

View Comments